February 24, 2014

Kumekucha Tamasha la Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
 Baadhi ya watazamaji wakifuatilia moja ya maonyesho ya tamasha hilo
 Moja ya kikundi cha Sanaa cha acrobat kikionyesha uwezo wao wa sanaaa hiyo 2013
 Kikundi cha Sanaa cha TaSUBa wakifanya vitu jukwaani kwenye moja ya tamasha hilo 2013. jukwaani
Moja ya vikundi vya kigeni kutokka Norway kikiwajibika jukwaani 2012.

 Na Andrew Chale, Bagamoyo

TAMASHA la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo kwa mwaka huu (2014) litakuwa la 33, ambapo linatarajia kulindima kwa siku saba, kuanzia Septemba 22 hadi 28, kwenye viunga vya  Chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Tamasha hilo la 33, mwaka huu, lenye kauli mbiu, “Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii”,  limekuwa msaada mkubwa  kwa wasanii na vikundi mbali mbali kujitangaza kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa fursa za kibishara katika kipindi chote cha tamasha.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Bafadhil ‘Bura’, alieleza kuwa, tayari mipango  na maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea katika kufikia malengo  huku akiwaomba wadau kujitoakeza na kudhamini tamasha hilo.

 “Milango ipo wazi hivyo, kwa wadhamini kujitokeza na kuchangamkia fursa hii hadimu, kwani tamasha hili ni kongwe katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla” alisema Bura.

Na kuongeza kuwa,  tamasha hilo lenye mvuto wa kipekee ndani na nje ya Tanzania, limekuwa likipata umaarufu mkubwa kila mwaka kutokana na idadi kubwa ya watazamji wa ndani na wale wa kutoka Mataifa mbali mbali duniani.

Kwa upande wake, Katibu wa tamasha hilo, Benjamini Mahimbali alieleza kuwa, tamasha hilo limekuwa na mafanikio ikiwemo ongezeko kubwa la watazamaji na vikundi vinavyoomba kufanya maonyesho.

“Idadi ya watazamaji na imekuwa ikiongezeka kila mwaka, huku kwa mwaka jana tulikuwa na wastani wa watazamaji elfu nne mia saba kwa siku (4,700), ikiwemo wa rika zote.” Alisema Ben.

 Na kuongeza kuwa, wanatarajia ongezeko hilo kuwa kubwa zaidi kutokana na maboresho na mipango mbali mbali inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Katika tamasha hilo maonyesho mbali mbali yanatarajiwa kuonyeshwa ikiwemo; Muziki wa aina tofauti, ngoma, maigizo, sarakasi, mazingaombwe na maonyesho kemkem ya sanaa na utamaduni wa Mtanzania na ya Mataifa mengine duniani.

Kwa upande wa fomu za kushiriki tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu wanatarajia kupokea vikundi zaidi ya 40,  zinatarajiwa kutolewa kwenye ofisi za Chuo hicho pamoja na tovuti ya chuo (www.tasuba.ac.tz)

No comments:

Post a Comment

Pages