February 16, 2014

MAMA TUNU PINDA:  MTAJI WA VICOBA NCHINI UNAKUA KWA KASI SANA
“Takribani shilingi bilioni 100/- kwa mwaka”
MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda (pichani), amesema miongoni mwa mifumo ya fedha inayo kuwa kwa kasi hapa nchini ni VICOBA.

Alisema hayo katika Kata ya Kimanga jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizindua rasmi muungano wa VICOBA wenye vikundi 46 na vikundi 25 vyenye jumla ya wanachama 600 ambao ndio waliopo katika mchakato wa muungano huo.

Mfumo wa VICOBA umeendelea kushamiri na kuenea katika maeneno mbalimbali nchini ambapo wananchi wengi hasa wa kipato cha chini na  asilimia kubwa wakiwa kina mama wameweza kunufaika na mfumo huu:

 “Inakadiriwa kuwa takriban asilimia 35 ya wananchi Kitaifa wanatumia huduma za fedha zisizo rasmi ambazo ni pamoja na VICOBA” alisema.

Mama Pinda aliongezea kuwa, taarifa  hizi  zinawapa  faraja  hasa kina Mama kwa kuona kuwa Serikali yetu inatambua Mfumo wa VICOBA na ambao umedhihirishwa  kuwa  wa  Mafanikio makubwa.

“Ni matumaini kwamba Serikali yetu imejipanga vizuri kusaidia upatikanaji  wa  huduma  za  fedha  kwa njia ya VICOBA kwa Watu wenye kipato cha chini na hasa Wakina Mama alifafanua Mama Pinda”.

Mama Pinda alisema, ninayo taarifa kwamba tayari Serikali yetu imekwishatoa maelekezo kwa kila Halmashauri kuhakikisha, Wanachama wa VICOBA wanapata mafunzo ya kuwapa uelewa wa dhana na Mfumo wa VICOBA ikiwa ni pamoja na jinsi vinavyoendeshwa na namna ya kujiendeleza: 

“Matarajio yangu ni kwamba maelekezo hayo ya Serikali yatawasaidia katika Vikundi vyenu mnavyovianzisha viwe na ubora zaidi na hatimaye kujikomboa katika umaskini wa kipato”alisisitiza.

Mama Pinda aliwashauri wana VICOBA kuangalia namna ya kuongeza hisa na michango kwa kila mwanachama ili kikundi kiweze kukua, kwani shilingi elfu 2000 kwa kununua hisa, shilingi 1000 kuchangia mfuko wa jamii na shilingi 500 kuendesha kikundi pamoja na shilingi 500 kwa ajili ya kumkopesha mwanakikundi endapo atakuwa na matatizo bado ni viwango vidogo kuendanda na hali halisi ya gharama za maisha na mahitaji.

“Natoa  rai kwa wataalamu wa Benki, NSSF na Mifuko mingine wakishirikana na Serikali kutoa elimu ya VICOBA ili vikundi hivi viweze kujiimarisha” alisisitiza.

Miongoni mwa changamoto wanazokutana nazo wana vikundi hao wa VICOBA Kata ya Kimanga ni pamoja na uelewa mdogo wa wanavikundi kuhusu VICOBA na taasisi za fedha kudai riba kubwa kwenye mikopo.

No comments:

Post a Comment

Pages