February 16, 2014

WAKAZI WA JIJINI DAR WAILALAMIKIA DAWASA

Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wakazi wa maeneo ya jiji la Dar es Salaam wameilalamikia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA), kwa kushindwa kwake kutengeneza mifereji ya majitaka ambayo imeharibika kwa muda mrerefu huku ikitiririsha maji hayo holela mitaani.

Wakazi hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa mifereji hiyo imekuwa ikitililisha vinyesi hivyo kwa zaidi ya mwezi bila mamlaka hiyo kuchukuwa hatua ya kuwaondolea kero hiyo.

Waliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na kadhia hiyo kuwa ni barabara ya uhuru karibu na jengo lililoko kitalu namba 13, maeneo ya Posta mpya ambako kuna zaidi ya mifereji mitatu.

Eneo lingine ni Kisutu Sokoni ambako wafanyabiashara na baadhi ya wateja walidai kuwa mfereji huo umekuwa ukitiririsha kinyesi zaidi ya mwezi sasa bila ya wasika kuchukua hatua.

Mmoja wa Wafanyabiashara sokoni hapo, Hamza Bomboko alisema kutiririka kwa kinyesi katika mfereji huo kumeanza muda mrefu hata kabla ya mvua zinazoendelea kunyesha sasa.

“Naweka tahadhari wasije wakasema hali hiyo imesababishwa na mvua hapana mfereji huu umezibuka muda mrefu sana kabla ya mvua hizi kuanza kunyesha,”alisema Bomboko.

Alisema wamezunguukwa na hatari kwani kinyesi hicho wakati mwingine kikikanyagwa na baadhi ya magari yanayopita kwa kasi kinaruka na kusambaa hadi kwenye biashara zao hali inayohatarisha maisha yao pamoja na wateja kupatwa na maradhi ya mlipuko.

Alipotafutwa Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasa, Injinia Boniphace Kasiga, ili kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko hayo, alisema kuwa wao ni wamiliki wa utoaji huduma wa mifereji hiyo katika miji, kazi ya uendeshaji si yao.

Alisema kazi ya kuendesha shughuli za kutoa huduma ya majisafi na majitaka, kutoa Ankara za wateja na kukusanya maduhuli na kuunganisha maji kwa wateja wapya wahusika ni Dawasco.

Kasiga, alisema kazi nyingine ya Dawasa ni kusimamia matengenezo makubwa ya miundombinu yote pindi watakapolekewa taarifa na waendeshaji (Dawasco), ambako gharama zinakuwa juu Dawasa.

No comments:

Post a Comment

Pages