United Republic Of Tanzania
Tanzania Communications Regulatory Authority
Mnamo mwezi Julai, 2013, Serikali
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilikamisheni jopo la wataalamu
wa Chuo Kikuu kufanya tathmini ya mchakato mzima wa uhamaji toka mfumo wa
utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa kidijiti pamoja na uzimaji wa mitambo
hiyo kwenye miji saba ambayo ni Dar e
salaam, Tanga, Moshi, Mwanza, Dodoma, Arusha na Mbeya. Uzimaji wa mitambo
ya analojia ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria, ambayo iko kwenye kanuni
zinazojulikana kama “Digital Broadcasting and Other Networks 2011”
Jopo hilo lilijumuisha wataalamu
wafuatao:-
Prof. Nerey
Mvungi Mtaalamu wa Mawasiliano ya
ki electronic
Dr.Francis
Sichona Mtaalamu wa Takwimu
Mr.F.M
Ishengoma Mtaalamu wa Habari na
Mawasiliano
Wote hawa ni wafanayakazi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
1.1
MADHUMUNI YA TATHMINI
Madhumuni ya tahmini hii ilikuwa
imejengwa kwenye maeneo Makuu manne kama ifuatavyo;
(a) Tathmini ya utendaji na utoaji huduma
za utangazaji kwenye mfumo wa kidijiti ikiwa ni pamoja na usimikaji wa miundo
mbinu ya kidijiti.
(b) Tathmini ya kuangalia jinsi Mamlaka
ya Mawasiliano ilivyokuwa imejizatiti kuandaa na kusimamia zoezi zima la
uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijiti
(c) Tathmini ya jinsi watumiaji wa huduma
za utangazaji walivyopokea mabadiliko hayo na changamoto zilizopo na
(d) Tathmini ya jinsi zoezi zima la
uzimaji mitambo lilivyoendeshwa.
Katika uendeshaji wa tathmini hiyo
wataalamu walizingatia mambo muhimu yafuatayo ikiwa ni pamoja na hoja
zilizotolewa na taasisi na watu mbalimbali kutoka kwenye jamii kama ifuatavyo:-
(i)
Idadi
ya visimbuzi vilivyokuwepo kwenye soko kabla ya uzimaji mitambo kama
vinatosheleza mahitaji,
(ii)
Idadi
ya watu walioweza kununua visimbuzi ilikuwa ndogo hivyo watu wengi kushindwa
kununua na kukosa habari zinazopatikana kwa njia ya luninga,
(iii) Ushirikishaji wa wadau kwenye
mchakato mzima wa uhamaji toka mfumo wa analojia kwenda kidijiti kabla ya
uzimaji mitambo hiyo,
(iv) Kiwango cha Elimu kwa Umma (Public
Awareness Campaign) kilichotolewa kabla na baada ya uzimaji mitambo,
(v)
Bei
za visimbuzi kama zilikuwa juu kwa watu wa hali ya kawaida na kusababisha
kushindwa kuvinunua,
(vi) Ubora wa visimbuzi na upokeaji wa
matangazo usioridhisha kama vile kuganda kwa picha.
1.2
NJIA ILIYOTUMIKA KUFANYA TATHMINI
Njia iliyotumika kufanya tathmini hii
ni ile inayotumika kimataifa (International Best Practise) kuendesha mazoezi
kama haya ijulikanayo kama “Sampling Approach” ambapo takwimu hukusanywa kwa
kuzingatia uwiano wa kaya zilizopo kwenye eneo husika, jinsia, umri, elimu na
kazi za kumuingizia kipato mtu anayehojiwa.
Makundi mabalimbali yanayohusika
kwenye mchakato huu wa uhamaji kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali
yalihojiwa kwa kupitia dodoso maalumu lililoandaliwa na maoni yao yalikusanywa.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i)
Watumiaji
wa huduma ya matangazo kwa mfumo wa kidijiti (Consumers)
(ii)
Watengenezaji
na wasambazaji wa maudhui kwa njia ya Luninga (Content Service Providers)
(iii)
Wasimikaji
wa miundo mbinu ya kidijiti (Multiplex Operators) na
(iv)
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania.
2.0
MATOKEO YA TATHMINI
Yafuatayo ni matokeo ya zoezi zima la
tathmini hiyo kama ilivyoendeshwa kwenye maeneo tajwa hapo juu.
2.1
TATHMINI YA UTENDAJI NA UTOAJI HUDUMA
ZA UTANGAZAJI KWENYE MFUMO WA KIDIJITI IKIWA NI PAMOJA NA USIMIKAJI WA MIUNDO
MBINU YA KIDIJTI.
Tathmini iliyoendeshwa na jopo la
wataalam kuhusu utendaji na huduma kwa walaji kwa ujumla wake zimeonyesha
yafuatayo;
(a)
Asilimia
89% ya kaya za watumiaji (consumers) walikuwa wakitumia huduma ya matangazo kwa
mfumo wa kidijiti mara baada ya uzimaji wa mitambo ya analojia kwenye miji saba
ambayo tathmini ilikuwa ikifanyika
(b)
Asilimia
11% ya kaya za watumiaji hawakuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu
mbalimbali kama ifuatavyo:-
-
5.5%
hawakununua visimbuizi
-
0.1%
ya Kaya, walisema visimbuzi vilikuwa havipatikani
-
3.2%
ya Kaya, walishindwa kunua visimbuzi sababu ya bei kuwa juu
-
0.2%
ya Kaya visimbuzi vyao vilikuwa vibovu
-
0.3%
ya Kaya, visimbuzi havikuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu ya
mawimbi hayapatikani kwa ubora zaidi (Poor signal reception)
-
0.9%
ya Kaya Luninga (TV screen) zilikuwa mbovu
-
0.7%
ya Kaya hawakuwa na umeme
2.2
UTAYARI WA MAMLAKA YA MAWASILIANO
KUANDAA NA KUSIMAMIA ZOEZI ZIMA LA UHAMAJI TOKA UTANGAZAJI WA MFUMO WA ANALOJIA
KWENDA KIDIJITI
Jopo la wataalamu lililokuwa likiendesha tathmini hii
liliweza kuthibitisha kuwepo kwa mambo yafuatayo pamoja na baadhi ya nyaraka
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA):-
-
Kuwepo
kwa kamati ya Kiufundi inayoundwa na wadau mbalimbali ikiwa na kazi ya kutoa
ushauri wa kiufundi kwa maswala yote yanayohusu uhamaji toka utangazaji wa
analojia kweda kidijiti,
-
Kuwepo
kwa dira madhubuti inayoonyesha mambo muhimu ya kutekelezwa kuelekea uzimaji wa
mitambo ya analojia,
-
Kuwepo
kwa sheria na kanuni zinazosimamia zoezi la uhamaji toka analoja kwenda
kidijiti,
-
Kuwepo
kwa nyaraka mbalimbali zinazoonyesha muhtasari wa vikao mbalimbali
vilivyofanywa kati ya wadau na Mamlaka ya Mawasiliano.
Vilevile Jopo la wataalamu
liliweza kuthibitisha mambo yafuatayo:-
-
Muundo
bora wa leseni unaozingatia utoaji huduma za matangazo ya kidijiti,
-
Utaratibu
mzuri wa ushindani kwa njia ya wazi uliotumika kuwapata “Multiplex Operators”
(wajenga Miundombinu na Wsambazaji wa matangazo),
-
Waraka
unaonyesha mchakato wa namna ya kupata malipo yananayotakiwa kulipwa na
watengenezaji na wasambazaji wa maudhui
(Transmission fee) kwa wenye leseni ya miundo mbinu ya kidijiti (Multiplex
Operators),
-
Mfano
wa nyaraka itakayotumika kufikia makubaliano ya utoaji huduma na mahusiano yao
kibiashara (SLA) kati ya wasimikaji wa miundo mbinu ya kidijiti na
watengenezaji na wasambazaji maudhui.
Kutokana na vielelezo na nyaraka
ambazo jopo la wataalamu iliweza kuzipata, jopo limeridhika kabisa kuwa Mamlaka
ya Mawasiliano ilikuwa imejizatiti vizuri kuandaa na kusimamia utekelezaji wa
uhamaji toka mfumo wa zamani wa analojia kwenda utangazaji wa mfumo mpya wa kidijiti.
2.3
MATOKEO YA TATHMINI KUHUSU
UPATIKANAJI WA VISIMBUZI NA ELIMU KWA UMMA
Tathmini imeonyesha kuwa kati ya kaya zote zilizohojiwa
kwenye miji saba, ni 0.1% ya kaya zilizodai uhaba wa visimbuzi wakati wa zoezi
zima la uzimaji mitambo ya analojia. Matokeo mingine ni kama ifuatavyo:-
-
35.4%
ya kaya zilizohojiwa walinunua visimbuzi kabla ya uzimaji mitambo ya analojia
na kabla ya kuanza utoaji wa elimu kwa umma kuhusu mfumo mpya wa uatangazaji wa
kidijiti
-
29.5%
ya kaya walinunua visimbuzi kabla ya uzimaji mitambo ya analojia lakini baada
ya utoaji elimu kwa umma
-
35.1%
walinunua visimbuzi baada ya uzimaji mitambo
Takwimu
hizi zinaonyesha kuwa upatikanaji wa visimbuzi na bei halikuwa tatizo kubwa lililoathiri mchakato mzima wa
uhamaji kutoka mfumo wa analojia
kwenda kidijiti kwenye miji hii saba. Vilevile elimu kwa umma ilisaidia sana
kuhamasisha walaji kuhamia kwenye mfumo huu mpya wa utangazaji
2.4
ZOEZI LA UZIMAJI MITAMBO YA ANALOJIA
Ilifahamika kuwa zoezi la uzimaji
mitambo ya analojia lilifanyika kwenye awamu nne ambapo kila awamu ilitoa
nafasi ya mwezi mmoja. Jopo la wataalam limeridhika na utaratibu huu, ambao
unatoa nafasi kubwa ya kutathmini matatizo yanayojitokeza kwenye awamu ya
kwanza kabla ya kwenda kwenye awamu nyingine. Vilevile ulitoa fursa ya
kuhakikisha kuwa eneo linalofuata linakuwa na visimbuzi vya kutosha na elimu
kwa umma inatolewa kikamilifu kwa kutumia Radio na Televissheni za eneo husika.
2.5
WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI MAUDHUI
(CONTENT SERVICE PROVIDERS)
65% ya watengenezaji na wasambazaji
wa maudhui walikuwa wamejiunga na mfumo wa kidijiti kabla ya uzimaji wa mitambo
ya analojia.
Sababu kubwa ya vituo vingine
kutojiunga na mfumo huu kwa wakati ilikuwa ni sababu za kimazoea kwamba huenda
mitambo isingezimwa kwa wakati uliopangwa.
Mpaka sasa vituo vyote vilivyopo Dar
es Salaam vimeshajiunga na mfumo huu kasoro kituo kimoja.
3.0
MAJUMUISHO
3.1
Jopo
la wataalam limeridhika kuwa watazamaji wengi waliokuwa kwenye mfumo wa
analojia walijiunga kwenye mfumo wa kidijiti. 11% tu ndio ambao hawakuweza
kujiunga kwa sababu mbalimbali kama nilizoelezea mwanzoni. Idadi hiyo inaweza
kuwa imepungua kwa vile watu wamekua wakiendelea kununua visimbuzi,
3.2
Zoezi
hili halijawanyima watanzania haki ya kupata habari kwani wengi tayari
wameshajiunga na mfumo huu mpya. Jopo liliona kuwa sababu ya malalamiko mengi
yalitokana na tabia halisi ya wanadamu kuogopa mabadiliko,
3.3
Kutokana
na takwimu zilizokusanywa, jopo limeridhika kabisa kuwa elimu kwa umma
ilitolewa kwa kiwango kikubwa kwani 90% ya kaya zilizotembelewa walikuwa na
habari kuhusu mfumo huu mpya wa utangazaji kwa njia ya kidijiti,
3.4
Hatua
madhubuti zilichukuliwa kuhakikisha kuwa kabla eneo husika kuzimwa mitambo ya
analojia kulikuwa na visimbuzi vya kutosha,
3.5
Mfumo
huu mpya wa kidijiti utatoa fursa nzuri kwa watengenezaji na wasambazaji wa
maudhui kutumia muda wote kutengeneza vipindi vizuri badala ya kujihusisha na
usimikaji miundo mbinu ya utangazaji,
3.6
Mfumo
huu mpya wa utanagazaji kwa njia ya kidijiti umeongeza ubora wa picha na
channel nyingi. Juhudi zifanyike kuwa na channel nyingi za nyumbani badala ya
nje ya nchi.
3.7
Jopo
limeridhika kuwa mfumo huu mpya haujapunguza idadi ya watazamaji wa luninga ila
watazamaji wamegawanyika kutazama channel mbalimbali na hivyo kujenga hisia
kuwa watazamaji wamepungua.
3.8
Maeneo
mengi yaliyokuwa yanapokea channel moja mpaka tatu sasa wanaweza kuona channel
za kinyumbani zaidi ya tano.
3.9
Uhamaji
kutoka DVB-T kwenda DVB-T2 uende kwa nguvu ya soko kwani dhana nzima ilikuwa
kuhama mfumo wa analojia kwenda kidijiti, na viwango vyote hivi viwili vinatoa
matanagazo ya kidjiti
4.0
HITIMISHO
Kutokana na matokeo ya tathmini iliyofanyika serikali
inashauriwa iendelee na zoezi la uzimaji mitambo ya analojia sehemu
zilizobakia. Jopo limeridhika na uandaaaji na usimamizi wa zoezi hili na kwamba
kasoro zilizojitokeza ni sababu ya hofu ya mabadiliko na uzoefu wa walaji
kwenye matumizi ya visimbuzi. Vilevile kuna faida nyingi za mfumo wa kidijiti
ambazo watoa huduma wanatakiwa kuzitumia ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Serikali inashauriwa kutoa punguzo la kodi kwa visimbuzi
ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kununua visimbuzi na kupata habari kwa
njia ya Luninga
Naomba niwakabidhi ripoti hii ambayo ina maelezo na
taarifa za kina kuhusu zoezi tathmini hii.
Imetolewa na:
Prof. Nerey Mvungi Mtaalamu wa Mawasiliano ya ki
electronic
Dr.Francis Sichona Mtaalamu wa Takwimu
Mr.F.M Ishengoma Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano
JOPO LA WATAALAMU
TOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
19 FEBRUARI 2014
No comments:
Post a Comment