HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2014


TIC ILIVYOSHIRIKI KONGAMANO LA UWEZASHAJI JIJINI MWANZA
 Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki wakati alipotembelea Banda la Kituo hicho kwenye Maonyesho ya Kongamano la Uwekezaji yaliyoanza jana kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (katikati) akisaini Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ,wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Yohana Balele (kushoto).Wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri.na Kulia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akibadilishana Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki mara baada ya kusainiana na wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,jijini Mwanza jana.Shughuli hii imefanyika wakati wa Muendelezo wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akizungumza wakati alipokutana na baadhi ya wawekezaji wenye leseni za TIC (hawapo picnani) ,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Jijini Mwanza jana.
Mmoja wa Wawekezaji waliopo ndani ya Kanda ya Ziwa,akiwasilisha jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki. Picha Zote na Othman Michuzi, Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages