BAADHI
ya vijana nchini wamewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupigania ili
tunu za taifa ziongezwe katika Ibara ya kwanza kifungu cha tano.
Tunu
ambazo wametaka ziongezwe ni ardhi na amani.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, vijana hao
walisema bila ya kuwa na utaratibu maalumu wa umiliki wa ardhi kuna hatari nchi
kuingia kwenye machafuko.
Walisema
wamefikia hatu hiyo baada ya kubaini vifungu
hivyo muhimu vimeachwa kwenye rasimu ya pili ya katiba itakayoanza
kujadiliwa bungeni kesho.
Mmoja
wa vijana hao, Amos Joseph, alisema ardhi na amani ni vitu muhimu kwa maisha ya
Watanzania, hivyo kutofanywa tunu za taifa ni jambo la hatari.
“Rasimu inatamka Jamhuri ya Muungano itaenzi
na kuzingatia Tunu za Taifa ambazo ni utu, uzalendo, uajibikaji, umoja, uwazi
uwadilifu na lugha ya taifa, huku ardhi na amani vikiachwa na ambavyo ni vitu
muhimu katika mustakabali wa nchi yetu,”alisema Joseph.
Matrida
Thobias, ambaye ni mlemavu wa kutosikia (kiziwi), mkazi wa Mabibo, alisema
pamoja na kuwa Watazania bado wanaendelea kuienzi amani na kuilinda ,lakini
anaamini umefika wakati wa amani kuingizwa kwenye kifungu hicho.
Alisema
machafuko mengi wanayoyasikia yakitokea
kwenye baadhi ya nchi duniani yamekuwa yakichangiwa na amani kutofanywa
kuwa Tunu ya Taifa.
No comments:
Post a Comment