HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2014

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

 Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro. (Picha na Dixon Busagaga)
 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Elinas Palangyo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devota Mdachi, Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete na Afisa Utalii Antipas Mgungusi.
 Wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid pamoja na wenzi wao wakiwa Hifadhi ya Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro.
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Na Dixon Busagaga, Moshi

SHIRIKA la hifadhi za taifa (TANAPA) limesema ujio wa magwiji wa klabu ya Real Madrid kutembelea hifadhi ya mlima huo pamoja na vivutio vingine vya utalii ni fursa muhimu katika juhudi za kutangaza mlima huo na kuongeza idadi ya Watalii .

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya magwiji hao
walipotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro Meneja
Mawasiliano wa shirika hilo Pascal Shelutete alisema ziara hiyo
itasaidia ongezeko kubwa la watalii kutoka  nchi za Hispania,Ufaransa
na kote ulimwenguni.

"Tumendika historia mpya kwa wachezahji wa zamani wa Klabu ya Real Madrid ya kule Hispania kutembelea hifadhi ya mlima Kilimanjaro, Kama TANAPA tunaamini ziara hii kuja na kupanda mlima Kilimanjaro, itasaidia kwa kiwango kikubwa sana kuongeza idadi ya watalii kutoka kote ulimwenguni,”alisema Shelutete.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama katika risala yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Rombo, Elinasi
Pallangyo alisema mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na TANAPA unaamini wacheaji hao watakuwa ni mabalozi wazuri wa kutangaza mlima huo kimataifa.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kiongozi wa msafara wa wakongwe hao kupanda mlima Kilimanjaro, Ramon Cobo, alisema kutokana na kile walichokishuhudia juu ya mlima huo, wanaahidi kuwa mabalozi wa Mlima huo watakapofika nyumbani kwao.

"Tumefurahi sana kupanda Mlima Kilimanjaro, tumejionea vitu vingi, ni mlima wa ajabu sana, tunaamini tutakapofika nyumbani kwa umoja wetu na umaarufu tulionao kama wachezaji wa klabu maarufu duniani tutakuwa mabalozi wa mlima Kilimanjaro," alisema Cobo.

Kundi la wachezaji hao  waliopata kutamba na Klabu ya Real Madrid
walipata bahati ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi yalipo maporomoko ya maji na baadaye kurudi ambapo wote walikabidhiwa vyeti maalumu vya kushiriki kupanda mlima huo toka hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Ugeni huo ulipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro KIA,majira ya saa 5:30 wakiwa na ndege ya shirika la ndege la Fast Jet ambapo walilakiwa na mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo pamoja na wenyeji wao klabu ya soka ya Panone fc.


Baadaye wakongwe hao walielekea katika Uwanja wa michezo wa Ushirika na kusghuhudia mchezo kati ya Mabingwa wa Kilimanjaro, Panone FC na Machava kabla ya kuondoka kuelekea mkoani Arusha ambako jana walitarajiwa kutembelea vivutio vingin evya utalii kama vile Ngororngoro na hifadhi ya Arusha.

No comments:

Post a Comment

Pages