October 10, 2014

WASANII MSIDANGANYIKE-BAVICHA

WASANII wametakiwa kutokubali kuingizwa mkenge kwa kudanganywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa Katiba inayopendekezwa inawatambua.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Edward Simbey, alisema ni lazima wawe makini uhuni huo wa CCM.
Alisema, Katiba hiyo ya CCM inaonekana kuwapa mamlaka wasanii lakini haiwapi haki ya kuidai mahakamani endapo watanyimwa, kwani imetamkwa wazi katika Ibara 27 ya Katiba.
Simbey, alisema kuwa katiba hiyo haitawasaidia chochote zaidi ya kuwakandamiza katika maslahi yao.

“Kwa kuwa kila walichotakiwa kukipata wakikosa hawatakuwa na haki ya kukidai popote pale,”alisema Simbey.

Alisema kilichofanyika katika katiba hiyo ni uhuni ambao na wao kama wasnii walitakiwa kuhoji nasio kushangilia, jambo ambalo litawaumiza miaka 50 ijayo.

No comments:

Post a Comment

Pages