October 08, 2014

CHUNGUZEN AFYA YA MACHO-CHAMA CHA MADAKTARI

Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Madaktari Bingwa wa Macho nchini kimewataka Watanzania kujenga tabia ya kuchunguza afya ya macho ili kuepuka upofu usio walazima.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama  hicho, Dk. Neema Kanyalu, wakati alipokuwa akizungumzia Siku ya Macho duniani, ambapo leo ndio kilele chake.
Alisema, kuna baadhi ya matatizo ya macho yanatibika kirahisi endapo mgonjwa atafika hosipital mapema na kfanyiwa ucgunguzi wa afya jicho. 
“Macho ni kiungo muhimu katika mwili kama vilivyo vingine kwa binadamu, ambapo yakipata matatizo ni vema mgonjwa akamwone daktari kwa ajili ya kupata tiba, na hata kwa wagonjwa wa kisukari, nao wanapaswa kuwaona watalaamu kwa ajili ya matatizo hayo ambayo husababisha macho kupata upofu.
“Matatizo ya macho yanatabi kinachohitajika ni kwa wagonjwa kujitahidi kufika katika hospitali mapema hali itakayowaidia kuwaepusha kupata upofu,”alisema Dk. Neema.

Dk Neema, alivitaja Vituo ambavyo vitahusika katika kutoa huduma ya uchunguzi wa macho na maradhi ya kisukari kuwa nikatika hospitali ya Ilala, Temeke na Mwananyamalautoaji.

Aidha, alitoa rai kwa wagonjwa wenye matatizo ya macho kuwa wanahakikisha wanapata matibabu kutoka kwa madaktari maalumu ambao walihusika na uchunguzi matatizo yao.

Dk Neema, alisema watakapofanya hivyo, itawasaidia katika kuwaepusha na matumizi ya dawa zisizo sahihi, hivyo kuwasababishia upofu baadala ya kuwaponya.

Vilevile, amewashauri baadhi ya akina dada nchini wanaopenda urembo kuwa makini na vitendo vyao uwekaji vioo bandia katika macho ili yabadilike rangi na kuwa kama ya wazungu kuwa ni hatari, kutawasababishia kupata upofu.


 Itakumbukwa kwamba, takwimu za WHO zilizotolewa hivi karibuni zinaonyesha asilimia 80 ya wagonjwa milioni 45 wa macho wana umri zaidi ya miaka 50 na asilimia 90 ya wagonjwa hao wanaishi katika nchi zinazoendelea zenye kipato cha chini ikiwemo Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages