October 08, 2014

MFUMUKO WA BEI UMEPUNGUA KWA ASILIAMI 6.7-NBS

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS),imesema mfumuko wa bei  katika kipindi cha Septemba mwaka huu umepungua kutoka asilimia 6.7 hadi 6.6 ikilinganishwa  na ilivyokuwa  mwezi Agosti.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za uchumi na Jamii, Ephraim Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka kutoka sh. 140.61 katika kipindi cha wa Septemba mwaka jana  hadi sh 149.9, Septemba mwaka huu.

Alisema hali hiyo imechangiwa na kupugua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha Septemba mwaka huu na Septemba ya mwaka jana.

“Hii inaamanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba mwaka huu imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka uliyoishi kipindi cha Agosti mwaka huu.

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi nao umepungua hadi asilimia 8.5 mwezi Septemba mwaka huu kutoka asilimia 8.8 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi Agosti mwaka huu,”alisema Kwesigabo.

Kwesigabo, alisema mfano, mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua katika kipindi cha Septemba 2014 zikilinganishwa na bei za Septemba mwaka jana kuwa ni pamoja na bei za mchele kwa asilimia 7.7, mahindi (asilimia 8.3), ulezi (asilimia 5.5), matunda (asilimia 5.0), na sukari.

Kwa upande mwingine, bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua bei katika kipindi cha Septemba mwaka huu zikilinganishwa na bei za Septemba mwaka jana ni pamoja na sare za shule kwa asilimia 4.9, simu za mkononi (asilimia 1.7, runinga (asilimia 2.8), na viatu (asilimia 1.2).

“Mfumuko wa bei wa Septemba mwaka huu unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.4 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 1.0 mwezi Agosti,” alisema Kwesigabo.

Aidha, uwezo wa sh 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh 66.70 katika kipindi cha Septemba mwaka huu kutoka Septemba mwaka 2010.

Akizungumzia mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, Kwesigabo alisema, unamwelekeo unaofanana na nchi nyingine.

Alisema mfano; mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua hadi asilimia 6.6 katika kipindi cha Septemba kutoka asilimia 8.36, 

Agosti mwaka huu na nchini Uganda uliendelea kupungua hadi asilimia 1.4 kutoka asimia 2.8 katika kipindi hicho hicho.

No comments:

Post a Comment

Pages