October 22, 2014

“COASTAL UNION KUIFUATA KAGERA SUGAR NA FAST JET"

Na Mwandishi Wetu, Tanga

MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania Bara mwaka 1988 Coastal Union “Wagosi wa Kaya”yenye maskani yake barabara 11 jijini Tanga inatarajia kutumia usafiri wa ndege aina ya fast Jet ikitokea  Dar kwenda mkoani Mwanza.


Baada ya kufika mkoani Mwanza itatumia usafiri wa basi kuelekea Bukoba ambapo watacheza mechi yao ya Ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar mechi itakayochezwa uwanja wa Kaitaba Bukoba.


Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa timu hiyo itaondoka mkoani hapa kesho asubuhi ikiwa na msafara wa
wachezaji,benchi la ufundi pamoja na viongozi mbalimbali wa timu hiyo.


Assenga amesema kuwa kuelekea mechi hiyo maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa lengo likiwa kuhakikisha timu hiyo inachukua pointi tatu muhimu kwenye mechi hiyo watakayocheza ugenini.


Akizungumzia hali ya kikosi cha timu hiyo,Kocha Mkuu Yusuph Chippo alisema kuwa wachezaji wote wapo kwenye hari kubwa ya kuelekea mechi hiyo wakiwa na matumaini ya kuweza kuibuka na pointi tatu muhimu.


Chippo amesema kuwa malengo yake makubwa katika michuano hiyo ni kuhakikisha wanamaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kwenye nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14.

No comments:

Post a Comment

Pages