October 05, 2014

DK. SLAA AITAKA SERIKALI KUBADILISHA MFUMO WA ELIMU


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akifafanua jambo katika sikukuu ya wahisani ya umoja wa wanafunzi wa kikatoliki (TYCS) iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mlezi wa umoja wa wanafunzi hao, Dustan Haule na Mwenyekiti, Johnson Kaaya. (Picha na Francis Dande)

Na Mwandishi Wetu
 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), D.k Willibrod Slaa ameitaka serikali kubadilisha mfumo mbovu wa elimu uliyopo sasa ili kuweza kuchenga taifa la wamisomi wailiyoelimika si bora wasomi.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, katika sikukuu ya wahisani ya umoja wa wanafunzi wa kikatoliki (TYCS), alisema kuwa msingi mmbovu wa elimu uliyopo ndiyo chanzo cha kuzalisha wasomi waliowengi lakini hawana sifa katika soko la Dunia.


“Mimi nashangaa kuona nchi hii, inabadilisha mfumo wa zamani ambao ulikuwa ukimfanya mwanafunzi kujisomea kwa bidii na kupata wasomi walio na maarifa na uchungu na nchi yao, lakini hivi sasa mwanafunzi analetewa mtihani wa kuchagua majibu, huu ni uzembe kwa mamlaka husika,” alisema.


Aliongezea kuwa, wazazi nao wanapaswa kuwafuatatilia watoto wao kwa ukaribu mkubwa katika masomo na maisha yao kwa ujumla, ili kuweza kutambua mapungufu ya mtoto na kuweza kuyatafutia ufumbuzi mapema.


Pia aliwataka wazazi, kuwapa fursa watoto endapo amengundua kuwa anakipaji na kuweza kukiendeleza kuliko kuona na kupuuzia jambo ambalo anauwa ndoto zao.


D.k Slaa, aliwataka vijana wote hususani wanafunzi, kutokujihusisha katika mambo mabaya yasiyompendeza mwenyezi Mungu yakiwemo Ulevi, Uzinzi, matumizi ya Madawa ya kulevya, rushwa na kuiga mambo ambayo hayana manufaa kwao ili kuweza kutimiza ndoto walizonazo kwa manufaa ya kwao na taifa kwa ujumla.


Naye Katibu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam TYCS, Yohana Deogratias alisema kuwa madhumuni ya umoja huo ni kuwasaidia wanafunzi kutambua haki na wajibu wao na kuweza kumjenga mwanafunzi kiroho.


Aliongezea kuwa, jimbo hilo lina jumla ya kanda 16 na matawi 250, pia aliwataka wakuu wa shule na walezi kuweza kuwaruhusu wanafunzi kuweza kushiriki matukio mbalimbali ya chama hicho ili kuweza kuwajenga kiroho.

No comments:

Post a Comment

Pages