October 06, 2014

WATANZANIA MSIWACHAGUE VIONGOZI MAFISADI-KASESELA

WATANZANIA wametakiwa kuwaadabisha kwa kutowachagua viongozi mafisadi wanaotaka kuingia madarakani kwa kutumia fedha chafu, katika chaguzi zijazo.

Kauli hiyo, ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela wakati wa ibada ya kuiombea nchi amani na mafanikio ya ujenzi wa Chuo cha Biblia mkoani Mbeya, yalifanyika katika Kanisa la Hossana Life Mission jijini Dar es Salaam.

Alisema endapo mafisadi hao wataingia madarakani katika cha guzi za Serikali za Mitaa zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni na uchaguzi mkuu mwakani, kuna hatari amani ya nchi ikatoweka.

Kasesera, alisema kiongozi yeyote anayeweka fedha mbele hawezi kusimamia utawala wa sheria ambao unaweza kusimamia utekelezaji wa haki, kitendo ambacho kitawasukuma wananchi  kutafuta haki yao kwa kutumia nguvu.

“Nchi inakabiliwa na viashiria vya uvunjivu wa amani kwa watu kunuka damu kwa mfano wapo watu wanawaua vikongwe bila hofu kwa imani za kishirikina hii ni ishara mbaya, nchi iliyozoeleka kuwa ya yamani na utulivu kumbe huku nyuma kuna kazi,”alisema Kasesera.

Alisema, jukumu la kulinda amani ni la wananchi wenyewe, na hiyo itawezekana pale watakapoamua kuchagua viongozi bora na wala sio mafisadi, akibainisha kuwa wanawajua wanaofaa na wasiofaa kwani watu hao wanaishi nao huko mitaani.

Akizungumzia Ujenzi wa Chuo hicho, Kasesela, alisema madhui yake ni mazuri ambapo pia alishauri kitakapokamilika kianzishe mafunzo ya upatanishi wa viongozi wa Afrika, kwani baadhi ya nchi viongozi wake wamejikuta katika migogoro ya kugombea madaraka na matokeo yake ni kuvuruguka kwa amani.

Kasesela japo fedha zinazohitajika katika ujenzi wa chuo hicho ni nyingi hata hivyo anaamini zitapatikana.

Awali, Askofu wa Kanisa hilo, Ephraim Mwansasu, alisema chuo hicho kitakapokamilika kitakuwa cha kwanza katia chi za Afrika zilizoko chini ya Jangwa la Sahara kwa kutoa mafunzo ya utambuzi wa Gharama ya Amani inapotoweka katika nchi husika.

Alisema wamefikia uwamuzi wakuwa na mafunzo hayo kwa sababu hivi sasa viongozi mbali wa dini na siasa wamekuwa wakiizungumzia uwepo wa amani lakini bila kutoa ufafanuzi kuhusu gharama zake katika maisha ya wananchi.

Katika rambee iliyofanyika Septemba saba mwaka huu jijini Dar es Salaam, Kanisa hilo lilikusanya sh milioni 100 wakati harambee hiyo ikiwa bado inaendelea katika makanisa mengine yaliyoko ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages