October 24, 2014

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA ENEO LA TANGANYIKA PAKERS AMBAPO NHC INATEKELEZA MRADI WA YUMBA WA KAWE CITY

1
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Felix Maagi akiiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati ilipotembelea eneo la mradi wa nyumba ambao unatarajiwa kuanza katika uwanja wa kulenga shabaha wa jeshi la wananchi Kunduchi, baada ya makubaliano kati ya jeshi la wananchi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake na jimbo la Kahama Mbunge Mh. James Lembeli na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka ilitembelea eneo hilo ili kujiridhisha na kujionea hali halisi na kupata maelezo ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo. Kulia ni Mjube wa Kamati hiyo Mh. Hamud Jumaa na Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, kulia ni James Lembeli Mbunge wa Kahama na Mwenyekiti wa kamati hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2
Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akielekeza jambo wakati alipokuwa akionyesha eneo hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na wajumbe wa kamati hiyo wakati alipotembelea eneo hilo huku Kunduchi. 3Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili Mh. Hery Shekifu akifafania jambo huku Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli wakimsikililiza 4Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la kulenga shabaha la jeshi Kunduchi, kulia ni Mama Zakhia Megji Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC na kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka 5
Baadhi ya watendaji na maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Kulenga Shabaha wa Jeshi Kunduchi ambao kwa sasa matumizi yake yanabadilisha na kuwa mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba.  7
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers ambapo mradi wa Kawe City unatarajiwa kuazishwa na shirika hilo la NHC.
 9
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo. 12
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli katikati ni mjumbe wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Hery Shekifu 13
Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akendelea kutoa maelezo kwa kamati hiyo wakati ilipotembelea katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe. 14Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo kabla ya kuanza ziara yao leo katika makao makuu ya shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam. 15Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipata maelezo ya awali kabla ya kutembelea maeneo yatakapotekelezwa miradi hiyo mikubwa ya makazi , Kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na kutoka kulia ni Mh. Mary Mwanjelwa mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum Mbeya mjini na Mh. Abdulkarim Shah Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo na na Mbunge wa Mafia. 17
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la NHC Mh. Zakhia Megji, Bw. Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi wa NHC na Mbunge wa jimbo la Ubungo na mjumbe wa kamati hiyo Mh. John Mnyika ambaye naonekana akitoa mchango wake wakati wa wajumbe hao walipokuwa wakipata taarifa ya awali..

No comments:

Post a Comment

Pages