October 23, 2014

Maabara za JK, ni Shubiri kwa Wananchi na Chadema?

Na Bryceson Mathias, Makuyuni-Korogwe

AGIZO la Rais Jakaya Kikwete la Ujenzi wa Maabara za Sekondari, Watendaji nchini wamelifanya Shubiri kwa Wananchi na hasa Wanachama wa Chadema wilayani Korogwe, ambapo Wawili kati yao wamewekwa ndani kwa kuhoji uhalali wa risiti Feki zinazotumika.

Kama lilivyokuwa Agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa Polisi Piga tu, Jumanne Billa, na Ibrahim Ramadhani wa Kijiji cha Gomba, wamewekwe ndani kwa kuhoji uhalali wa Risiti za Halmashauri anazotumia, Mtendaji Kata, Boniface Siluli, anayejiona ni Mungu Mtu kwa Watu.

Mtendaji alipohojiwa alisema, “Sifanyi kazi za Chadema, alipobanwa kwa lugha potofu alibadili., “nafanya kazi ya Wananchi, Kamuulize Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya”.alisema Siluli kwa simu 0713009002.

Mwandishi alimtafuta OCD Madulu wa Korogwe katika simu 0788637679, kama kuna Wanachama Wawili wa Chadema waliowekwa ndani, kwa kosa la kuhoji uhalali wa Risiti Feki za Michango ya Maabara, Magulu alisema hana taarifa hadi afuatilie ofisini kwake

Mwenyekiti wa Chadema Korogwe, Aulelian Nziku, alikiri Wanachama wake, Billa na Ramadhani, wa Gomba kuwekwa ndani Korogwe, baada ya kuchongewa na Mtendaji Siluli, kwa OCD Magulu na Mkuu wa Wilaya, kwa madai wanazuia Michango, na wakakataliwa dhamana.

Mwandishi anafanya Jitihada za kumpata Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, kama alitoa amri ya wanachama hao wa Chadema, wawekwe ndani kwa kuhoji Uhalali wa Risiti za Michango ya Maabara zinazolalamikiwa kuwa ni Feki, au lipo jambo lingine.

Kumekuwa na sintofahamu kwa wananchi, ya kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha zilizochangwa kwa ajili ya Maabara, na je risiti zinazotumika za Sh. 10,000/- kwa kila nyumba yenye Mwanamke na Mwanaume na watoto kuanzia miaka 18 ni halali au la?

“Wananchi tuna hofu kutokana na kutotangaziwa Mapato na Matumizi, ambapo kunatufanya tufikirie fedha zingine zitachotwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.alisema mmoja wao akikataa asitajwe jina akihofu kusurubiwa!

No comments:

Post a Comment

Pages