October 12, 2014

TIMU YA AMANI YAIIFUNGA TIMU YA MSHIKAMANO 1-0 KATIKA PAMBANO LA VIONGOZI WA DINI

 Wachezaji wa timu za viongozi wa dini wakifanya mazoezi mepesi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya mchezo maaalum uliowakutanisha viongozi wa dini.
Askofu wa Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa (kushoto), akifanya mazoezi mepesi na Msaidizi wa Askofu KKKT, Mchungaji George Fupe.

 Mwamuzi wa mchezo kati ya timu ya viongozi wa Dini ya Amani na Mshikamano, Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleima Kova akiingia Uwanja.
Waamuzi wa mchezo huo wakiingia uwanjani huku wakisindikizwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
 Mshambuliaji wa timu ya Mshikamano, Padri richard kamenya akimtoka beki wa timu ya Amani, Sheikh wa Bakwata, Khamis Mtonga 
 Benchi la Ufundi la timu ya Mshikamano.
 Kikosi kamili cha timu ya Mshikamano.
 Kikosi kamili cha timu ya Amani
Mechi Kamishna Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamSaid Mecky Sadick (katikati).
Mshambuliaji wa timu ya Mshikamano,Padri Richard Kamenya (katikati) akitafuta mbinu za kumfunga golikipa wa timu ya Amani, Sheikh Muharami Pembe wakati wa mchezo maalum uliowakutanisha viongozi wa dini na kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Kushoto ni Sheikh wa Bakwata, Khamis Mtonga.

No comments:

Post a Comment

Pages