October 10, 2014

Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa  kundi  namba 1 la  nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa  kundi  namba 1 la  nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa  kundi  namba 1 la  nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa  kundi  namba 1 la  nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Picha zote na Ingiahedi Mduma- Wizara ya Fedha.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA


Mkutano wa kundi  namba 1 la  nchi za Afrika- Benki ya Dunia
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika  hufanyika kila  mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka  IDA. IDA ni shirika au mfuko wa  maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.

Katika mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16.

Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka mwaka 2016. Mwaziri  wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni  MaGavana mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia.

Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema kuwa”tumepata  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka Zimbabwe “ alisema. 

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa  na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza.

Vilevile katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia  pamoja na Sierralion.

Jambo lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.

Vilevile walisisistiza suala la gonjwa  la EBOLA. Walielezea kuwa wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo tatizo.

Pia Benki ya Dunia  itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia ujuzi wanao upata. 

Mwisho walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa.
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi.

Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington D.C
9/10/2014

No comments:

Post a Comment

Pages