October 10, 2014

ROSE NDAUKA ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Na Mwandishi Wetu

MSANII mahiri wa filamu nchini, Rose Ndauka (pichani), mwanzoni mwa wiki alimliza mtangazaji Khadija Shaibu, maarufu kwa jina la Dida, wakati wa sherehe za kuazimishja siku ya kuzaliwa kwa msanii huyo.

Sherehe hizo zilifanyika katika Hoteli ya kifahari ya Correcium iliyopo maeneo ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na ndugu na jamaa wa Rose, wasanii mahiri kama Irene Uwoya, Single Mtambalike ‘Richie’, Maya, Shamsha Ford, Claud 112, Jacline Pentezel na wengineo.

Dida ambaye ndiye aliyekuwa mshehereshaji katika tukio hilo, alielezea jinsi Rose alivyowahi kumpigia simu Siku ya Wajinga Duniani, Aprili Mosi, akimwambia kuwa baba yake amefariki akilenga kumdanganya, lakini ikawa hivyo baada ya muda mfupi.

“Ni tukio ambalo sitaweza kulisahau, baba yangu alikuwa ni mgonjwa akiishi kwa akina Rose, Siku ya Wajinga Rose akanipigia simu akaniambia baba amefariki akilenga kunidanganya, baada ya muda akafariki kweli, kwa kweli niliumia sana na nadhani hili lilimuumiza sana mdogo wangu Rose,” alisema Dida na kuanza kuangusha kilio.

Kitendo kile kiliwafanya wote waliokuwapo ukumbini kupatwa na simanzi kutokana na kuguswa na maneno ya Dida.

No comments:

Post a Comment

Pages