October 05, 2014

MKUTANO WA WAHITIMU WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) WANAOISHI NYANDA ZA JUU KUSINI WALIO SOMA CBE KUANZIA MWAKA 1965-214 IKIWA NI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHUO JIJINI MBEYA

Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakangale (aliyesimama) akisoma hotuba yake katika Mkutano wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanaoishi Nyanda za Juu kusini waliowahi kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka 1965-2014 ambapo na yeye akiwa ni mmoja wa wanafunzi ambaye alisoma katika chuo hicho mwaka 1967.

Mh. John Mwakangale ambaye pia alikuwa ni Mkufunzi katika chuo hicho na Mlezi wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za Juu Kusini katika hotuba yake alikishukuru chuo cha CBE kwa kufanya mkutano huu muhimu wa kuwaalika wahitimu wote kukutana pamoja na kuongeza kuwa CBE ni chuo cha Kuigwa kwa sababu baadhi ya viongozi wamesoma katika Chuo hicho.

Baadhi ya viongozi hao ni Omar Kingi Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Stagomena Tax Katibu Mtendaji SADC, Harry Katillya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Suzan Kaganda-RPC Tabora, Dk. Ramadhani Dau Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na Graciano Kanzugala Mwenyekiti wa TCCIA Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Alimalizia kwa kuzindua umoja wa wanafunzi na kusema CBE ni chuo ambacho kimezalisha wataalam wengi. 
 Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile akisaini kitabu cha wageni wakati akiingia katika Mkutano huo.
 Mkuu  wa Chuo Cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya Ndugu Deonise Lwanga akitoa utambulisho pamoja na Kumkaribisha Mkuu wa Vyuo vyote vya CBE Tanzania.
 Mkuu wa Vyuo vyote vya Elimu ya Biashara (CBE ) Profesa Emmanuel Mjema akitoa nasaha zake na kueleza malengo makuu ya Mkutano huo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) , Mipango, Fredha na Utawala Dkt. Peter Msami akitoa Salamu za Shukurani kwa niaba ya chuo cha CBE.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo cha CBE Bwana John Mwangobola akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za juu Kusini ambao umezinduliwa Rasmi Tarehe 04.10.2014 Bwana Boyd Faustin Mwakyusa akitoa neno la Shukurani Baada ya uteuzi huo.
Msimamizi wa Taaluma kutoka Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya Bwana Kayombo akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo.
 Viongozi wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za Juu Kusini wakiwa pamoja na Mlezi wao Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile wa nne Kutoka Kushoto Mara baada ya Uchaguzi huo.
Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages