October 20, 2014

PHD: WAREMBO WA BONGO HAWANA JIPYA


NA ELIZABETH JOHN


STAA wa filamu za Bongo, Hemed Suleimani ‘PHD’  amesema kuwa amechoka na usumbufu wa warembo hapa bongo kwani hajaona jipya bali ni usumbufu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hemed alisema kuwa wasichana wamekuwa wakimsumbua kila kukicha wakiitaji kuwa naye hivyo ameona bora atafute msichana mmoja aweze kumuoa ili kuepukana na usumbufu huo.

Alisema kuwa yeye umri umeenda na wala haitaji usumbufu kwa wasichana wa kibongo bora kuoa ili waweze kupata heshima ya ndoa pindi anapokuwa na mkewe.

“Kwa sasa nahitaji kuoa kwani sijaona jipya kwa wasichana, sasa ili waweze kunieshimu bora nivute jiko niliweke ndani naona wasichana wataacha kunisumbua,”alisema

Alisema kuwa mpango wa kutafuta jiko ushakamilika na kwa sasa
anaanza maandalizi ya ndoa muda ukifika atawambia anaoa lini na kudai mtoto anayemuoa ni mkali sana.

Licha ya kuwa msanii wa filamu, msanii huyo pia anatamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya. 



No comments:

Post a Comment

Pages