October 18, 2014

VIONGOZI WIZARA YA FEDHA WAKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA

Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dk. Servacius Likwelile, ambapo ujumbe kutoka Tanzania ulikutana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier hawapo kwenye picha kwa madhumuni ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Bw. John Cheyo ambaye ni Kamishna wa Bajeti, anayefuatani Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Bi Amina na wa kushoto kwake ni Bw. Said Magonya ambaye ni Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dk. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekezwa na Benki ya Dunia kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier.
 Dr. ServaciusLikwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kulia ni Gavana wa Benki kuuya Tanzania na kutoka kushotoni  Bi. Natu Mwamba Naibu Gavana wa Benki Kuuya Tanzania wakimsikiliza kwa makini Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi hayupo kwenye picha, alipokuwa akijibu hoja zilizowekwa mezani.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi, Bw. Phippe Dongier alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Dk. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali na kuahidi kuzifanyiakazi.

No comments:

Post a Comment

Pages