October 18, 2014

Wasanii waaswa kuchangamkia kilimo Kwanza

Na Mwandishi Wetu
 
MCHUNGAJI wa Kanisa la KKKT, John Solomoni, ameshangazwa na kitendo cha idadi ndogo ya wasanii kujitokeza katika kununua mashamba ya bei rahisi yanayotolewa na Shirikisho la wasanii Tanzania(SHIWATA( yaliyopo Kijiji cha Ngarambe Wilayani Mkuranga.

Solomoni  ambaye pia ni Katibu wa kamati ya amani ya viongozi wa Dini mkoa wa Dar es Salaam,aliyasema hayo juzi katika hafla ya kuoneshwa mashamba kwa wasanii hao iliyoendana sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema kitendo kilichofanywa nawasanii inaonesha ni jinsi gani bado haewajaanza kujitambua katika kutengenezamaisha yao ya mbeleni.

Alisema kiasi cha shilingi 200,000 kinachotozwa kwa ajili ya msanii kupata ekari moja na nusu ni kidogo sana ukilinganisha na thamani ya ardhi ilivyo sasa lakini anawashangaa kwa nini wasanii wameshindwa kujitokeza kama ilivyotarajiwa.


“Hapa nimeambiwa shirikisho lina wasanii zaidi ya 8000 wakiwemo wasanii wakubwa wenye majina lakini kwa nini ni 95 tu ndio wanunue mashamba hii ni aibu na kushindwa kujitambua nyie ni kina nani mbele ya jamii,”alisema Mchungaji Solomon.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga,Saada Mwaruka, alisema kama Wilaya watawapa ushirikiano wa hali na mali wasanii waliochukua mashamba hayo ikiwemo kuwakopesha pembejeo za kilimo.

Mwaruka alisema wanataka waone  eneo hilo linakuwa shamba darasa la kuigiwa mfano jambo litakalowaamsha vijana wa Mkuranga nao kujishughulisha na kilimo na kuona kilimo sio kazi ya waliokosa kazi bali ni moja ya njia za kuwainua kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib, alisema  wameamua kubuni mbinu hiyo ili kuwaondoa wasanii wa nchi hii katika umasikini.

Taalib alisema katika mashamba hayo kuna jumla ya ekari 500 kwa ajili ya kulima huku awali walitangulia kagawa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba robo ekari kwa kila msanii lililopo maeneo ya Mwanzega huko huko Wilayani Mkuranga ili nao waweze kumiliki nyumba.

Alisema utaratibu huo ndio ulitumiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kuhamasisha vijiji vya Ujamaa ambako mpaka leo watu wameona matunda yake.

No comments:

Post a Comment

Pages