October 05, 2014

WALEMAVU WAOMBA ELIMU JUU YA KATIBA

NA Mwandishi Wetu
 
UMOJA wa Wafanyabiashara Walemavu Dar es Salaam (UWAWADA), umesema baada ya Bunge maalumu la Kutunga Katiba kumaliza kazi yake, kilichobaki sasa ni wananchi kupatiwa elimu ya kutosha iliwafanye maamuzi sasa hihi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa UWAWADA, Mohamed Kidumke, alisema ni vema Watanzania sasa wakaachwa waijadili Katiba hiyo inayopendekezwa ili waweze kujiua kilichomo ili waipigie kura kwa uhakika.

Alisema, elimu hiyo itawasaidia Watanzania kujua kama maoni yao waliyopendekeza wakati wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Jaji Joseph Wariyoba yameingizwa kwenye katiba hiyo iliyopendekezwa. 

“Serikali inabidi iongeze nguvu binafsi mpaka watu waelewe na kuweza kupiga kura,  kwa sababu wananchi wengi kama hawaikubali kutokana na kuona baadhi ya maoni yao ya muundo wa serikali tatu kuachwa na kurudishwa serikali mbili hali inayowafanya wananchi kugawanyika, hivyo elimu ya kutosha inahitajika,”alisema Mohamed.

Kidumke, lishauri serikali pamoja na vyombo vya dola kutoa uhuru kwa kila mwenye uwezo wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu katiba hiyo kwa sababu wengi bado hawajajua kilichopendekezwa na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba,
Aliongeza kuwa kama serikali itawanyima wananchi kujua kilichoandikwa kuana hatari wakaja wakafanya maamuzi ya kubahatisha kitendo ambacho hakina maslahi kwa Taifa.

“Wananchi tuachwe tufanye maamuzi wenyewe, wanasiasa, vyombo vya dola visituoingilie pindi wanapokuja watu kutupatia elimu,”alisema Kidumke. 

Akizungumzia kuhusu maoni yao kuingizwa katika katiba inayopendekezwa, Kidumke, alisema kwa kiasi kikubwa yameingizwa.
Alisema mjumbe wao alifanyakazi kubwa ya kusimamia maoni yao, na wanampongeza kwani alihusika katika kamati na hata kwenye uandikaji.

Kidumke, alisema katiba hiyo imegusa karibu makundi yote kama vile Watu wenye ulemavu, wakulima, wavuvi na wengine ambao baadhi ya taasisi zimesikika zikiipongeza.

Hata hivyo, alisema mvutano unaojitokeza kati ya vyama vya siasa na wanaharakati ni kawaida ya demokrasia, kwamba kila mtu anayo haki yakupendekeza anachotaka lakini mwisho wa siku sio rahisi kila maoni ya mtu kuingia kwenye katiba hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages