Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa
(Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya
kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa
ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi
wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF
zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa
Somhlolo jijini Mbabane.
MWAKIBINGA
AONDOKA BODI YA LIGI
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia
Bodi, na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
TPLB hivi sasa iko katika mchakato wa kupata
Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na
Mwakibinga baada ya muda wa mkataba wake kumalizika.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment