November 20, 2014

Mkwaja FC mabingwa wapya Mwidau CUP 2014

Na Mwandishi Wetu, Pangani

Timu ya soka ya Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliipigwa kwenye Uwanja wa Mwera wilayani Pangani.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika dakika za awali toka mpira kuanza.
Mchezaji wa Mkwaja FC Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya kwenda mapumziko . 
 Hata hivyo kipindi cha pili Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank kufanikiwa kufunga golo hilo baada ya kumhada mlinda mlango wa Mkwaja.
Goli la pili la timu hiyo lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha magoli yote lakini shauku yao ilikwisha baada ya dk 80 Mkwaja FC kufunga bao la nne.
Akikabishi zawadi kwa washindi hao Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa timu ya Mkwaja FC walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000, kikombe kikubwa, medali za dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira.
Huku mshindi wa pili ambae ni Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo, medali ya shaba, seti moja ya jezi pamoja na mpira huku timu 40 zilizoshiriki zikipatiwa mpira na 16 zikipatiwa jezi seti moja moja.
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji vya soka  katika wilaya hiyo kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali hapa nchini.
Katika mchezo huo wa fainali ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote kutoka CUF.

No comments:

Post a Comment

Pages