Timu
ya soka ya Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014
baada ya kuifunga timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange
uliipigwa kwenye Uwanja wa Mwera wilayani Pangani.
Mchezo
huo ambao ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini
timu ya Kiman’ga ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya
magoli katika dakika za awali toka mpira kuanza.
Mchezaji
wa Mkwaja FC Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya
kuifungia timu yake mabao matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya
kwenda mapumziko .
Hata
hivyo kipindi cha pili Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika
bao la kwanza katika dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank
kufanikiwa kufunga golo hilo baada ya kumhada mlinda mlango wa Mkwaja.
Goli
la pili la timu hiyo lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta
matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha
magoli yote lakini shauku yao ilikwisha baada ya dk 80 Mkwaja FC kufunga
bao la nne.
Akikabishi
zawadi kwa washindi hao Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa
timu ya Mkwaja FC walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000,
kikombe kikubwa, medali za dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira.
Huku
mshindi wa pili ambae ni Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo,
medali ya shaba, seti moja ya jezi pamoja na mpira huku timu 40
zilizoshiriki zikipatiwa mpira na 16 zikipatiwa jezi seti moja moja.
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji vya soka katika wilaya hiyo kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali hapa nchini.
Katika
mchezo huo wa fainali ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa
Konde, Khatib Said Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote
kutoka CUF.
No comments:
Post a Comment