Meneja Msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, wakati wa kutangaza washindi
wa shindano la Bia ya Castle Lite Yatch Party. Jumla ya washindi 15 wamepatikana.
Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofray Makau. (Picha na Francis Dande)
Meneja Msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, wakati wa kutangaza washindi wa shindano la Bia ya Castle Lite Yatch Party. Jumla ya washindi 15 wamepatikana. Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofray Makau.
Meneja wa Castle Lite, Geofray Makau
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya kupatikana kwa
washindi wa shindano la bia ya castle lite Yatch party ambapo jumla ya washindi
kumi na tano nchi nzima wamepatikana. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Castle Lite, Victoria
Kimaro.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Jumla ya washindi kumi na tano wa shindano la Castle Lite Yatch Party wamepatikan na wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam muda kwa ajili ya Tamasha kubwa la ndani ya bahari litakaloendeshwa na kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lite.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saaam leo,
Meneja msaidizi wa Bia hiyo, Victoria kimaro alisema kampeni ya kuwasaka
washindi hao ilichukua takribani miezi mitatu ambapo iliendeshwa nchi nzima.
Bia ya Castle Lite, inazozalishwa na kusambazwa na Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) leo imefunga rasmi promosheni ya "Lite Up The Weekend"
ambayo imeendeshwa kwa muda wa miezi mitatu katika mikoa kadhaa ya hapa nchini Tanzania ambayo ni;
Mbeya, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam. Washindi walioshiriki katika promosheni
hii.
Alisema Bia hiyo iliweza kufanya promoshen hiyo kwa lengo
kuu la kuwazawadia wateja wake na watanzania kiujumla ili kuweza kukutana
pamoja na kufurahia kwa pamoja kwa kuweza kusherekea kwa kushiriki katika
tamashi hilo kubwa litakalofanyika katikati ya bahari ya Hindi sanjari na
burudani mbalimbali zitakazokuwepo.
Pamoja na burudani hizi lakini safari nzima ya washindi wetu
imegaramiwa ikiwa ni pamoja na malazi, chakula na mambo mengine mengi Zaidi.
Kwa upande wake Meneja wa Castle Lite, Bwana Geofray Makau
aliwapongeza washindi hao na kuwataka kwenda kuwa mabalozi wazuri wa bia ya
castle lite popote waendapo wakizingatia kwamba hii ndi bia pekee kuweza
kuendesha shindano la kipekee kwa kuwashindanisha kistarabu wateja wake na hatimae
kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu na kuhudhuria katika hili tamasha la
kipekee.
No comments:
Post a Comment