November 05, 2014

WATEJA 15 WAIBUKA KIDEDEA KATIKA SHINDANO LA CASTLE LITE

Meneja Msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, wakati wa kutangaza washindi wa shindano la Bia ya Castle Lite Yatch Party. Jumla ya washindi 15 wamepatikana. Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofray Makau. (Picha na Francis Dande)


Meneja Msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, wakati wa kutangaza washindi wa shindano la Bia ya Castle Lite Yatch Party. Jumla ya washindi 15 wamepatikana. Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofray Makau.
 Meneja wa Castle Lite, Geofray Makau akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya kupatikana kwa washindi wa shindano la bia ya castle lite Yatch party ambapo jumla ya washindi kumi na tano nchi nzima wamepatikana. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro.
 
 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Jumla ya washindi kumi na tano wa shindano la Castle Lite Yatch Party wamepatikan na wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam muda kwa ajili ya Tamasha kubwa la ndani ya bahari litakaloendeshwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lite.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saaam leo, Meneja msaidizi wa Bia hiyo, Victoria kimaro alisema kampeni ya kuwasaka washindi hao ilichukua takribani miezi mitatu ambapo iliendeshwa nchi nzima.
Bia ya Castle Lite, inazozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imefunga rasmi  promosheni ya "Lite Up The Weekend" ambayo imeendeshwa kwa muda wa miezi mitatu katika mikoa  kadhaa ya hapa nchini Tanzania ambayo ni; Mbeya, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam. Washindi walioshiriki katika promosheni hii.
Alisema Bia hiyo iliweza kufanya promoshen hiyo kwa lengo kuu la kuwazawadia wateja wake na watanzania kiujumla ili kuweza kukutana pamoja na kufurahia kwa pamoja kwa kuweza kusherekea kwa kushiriki katika tamashi hilo kubwa litakalofanyika katikati ya bahari ya Hindi sanjari na burudani mbalimbali zitakazokuwepo.
Pamoja na burudani hizi lakini safari nzima ya washindi wetu imegaramiwa ikiwa ni pamoja na malazi, chakula na mambo mengine mengi Zaidi.
Kwa upande wake Meneja wa Castle Lite, Bwana Geofray Makau aliwapongeza washindi hao na kuwataka kwenda kuwa mabalozi wazuri wa bia ya castle lite popote waendapo wakizingatia kwamba hii ndi bia pekee kuweza kuendesha shindano la kipekee kwa kuwashindanisha kistarabu wateja wake na hatimae kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu na kuhudhuria katika hili tamasha la kipekee.

No comments:

Post a Comment

Pages