HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 30, 2014

Bayport yamjaza manoti mwanafunzi wa MUCE

Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akifafanua jambo wakati wa makabidhiano ya hundi kwa  Kennedy Kaupenda (kushoto), Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. 
Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania,   Ruth Bura (kulia)  akimkabidhi hundi yenye thamani mil 3 Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake. 

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.

Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.

No comments:

Post a Comment

Pages