Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpandisha cheo koplo, Catherina Lange kuwa Sanjenti wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akimpandisha
cheo Koplo Catherine Lange, kuwa Sajenti wa Jeshi la Magereza baada ya kung’ara
katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya riadha yaliyofanyika katika nchi za Brazil,
China na Angola.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akimpandisha
cheo Koplo Catherine Lange, kuwa Sajenti wa Jeshi la Magereza baada ya kung’ara
katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya riadha yaliyofanyika katika nchi za Brazil,
China na Angola.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akipompongeza
mwanariadha, Catherina Lange baada ya kumpandisha cheo.
Catherina Lange.
Catherina Lange.
Catherina Lange akiwa amepozi.
NA ELIZABETH JOHN
KAMISHINA Jenerali wa Magereza (CGP), John Minja, amempandisha cheo mwanariadha wa mbio ndefu, Catherina Yuku kutoka cheo
cha CPL wa Magereza hadi SGT wa Jeshi hilo kutokana na juhudi binafsi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati
akimpandisha cheo hicho, Minga alisema ni kutokana na umahiri wake katika mchezo
huo tangu aanze kupata mialiko ya kushiriki mashindano ya kimataifa kupitia
Riadha Tanzania (RT) tangu mwaka 2011.
Alisema kwa mamlaka aliyonayo katika Jeshi hilo
kwa mujibu wa sheria ya Magereza ya mwaka 1997, kwa ushindi na sifa
alizoliletea Jeshi la Magereza na Taifa, anampandisha hadi ngazi hiyo katika
kutambua na kuthamini juhudi yake.
Alisema, mwanariadha huyo ameshiriki mashindano
ya Kimataifa mara 12 ambapo yalifanyika katika nchi za Brazil, China, Angola na
mikoa mbalimbali hapa nchini.
CGP Minja alisema mwanariadha huyo ana rekodi ya
kupata medali tisa; tatu za dhahabu, tatu za fedha na tatu za shaba na katika mashindano
ambayo hajapata medali, bado alishika nafasi ya nne na ya tano akipata medali
za ushindi.
“Mashindano aliyoshiriki yalishirikisha
wanaraidha kuanzia 95 hadi 23, 657, kiwango chake kinazidi kupanda kwani katika
mashindano ya Desemba 2014 yaliyofanyika Shanghai, China alishika nafasi ya
kwanza kati ya washiriki 23, 657 na katika Uhuru Marathon ya jijini Dar es Salaam Desemba
mwaka jana, alishika nafasi ya kwanza kati ya washiriki 520,” alisema.
Kwa upande wake, Catherina alisema kuwa anaushukuru
uongozi wa Magereza kwa kuthamini na kutambua mchango wake.
“Zawadi hii itanifanya nizidi kuongeza juhudi
katika mchezo huu, najisikia faraja sana kupewa kitu kama hiki na nawahaidi
kwamba zawadi hii itanifanya niendelee kufanya vizuri,” alisema.


No comments:
Post a Comment