Lilivyokuwa Tamasha la Pasaka mwaka
2000
Na Mwandishi Wetu
WAKATI tukielekea kwenye Tamasha la
Pasaka ambalo linatarajia kufikisha miaka 15 tangu kuasisiwa kwake,
tujikumbushe baadhi ya matukio ambayo yaliyotokea katika matamasha yaliyopita.
Kwa kuwa lilikuwa ni tamasha la mwanzo
ambalo liliandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions yenye maskani yake Kinondoni
jijini Dar es Salaam, kulikuwa na changamoto nyingi kwa sababu ya ugeni katika
uandaaji wa matamasha.
Mojawapo ya changamoto zilizojitokeza
katika tamasha la kwanza ni kuzuiwa na
wamiliki wa ukumbi wa Diamond kwa deni la shilingi 300,000 ambazo zililipwa
baadaye.
Kadri miaka inavyokwenda mbele, Kampuni
ya Msama inapiga hatua taratibu kwa sababu ya ufanisi wa Kamati ya Maandalizi.
Katika tamasha hilo la kwanza mgeni
rasmi alikuwa rais wa awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi , hafla iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waimbaji waliopanda jukwaani
mwaka huo ni Marehemu Angela Chibalonza,
Kwaya ya Lulu Mtoni, Jangala Son, Mzungu Four na Faustine Munishi ambaye anaendelea na shughuli zake nchini
Kenya.
Itaendelea wiki ijayo…..
No comments:
Post a Comment