Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI
nguli wa Nyimbo za Injili barani Afrika raia wa Afrika
Kusini, Sipho Makhabane amepata ajali
nchini humo akielekea studio kwa ajili ya kazi za muziki.
Makhabane
alipata ajali hiyo akiwa kwenye gari aina ya Mercedece Benz ambako katika ajali
hiyo amepata majeraha kichwani na kukimbizwa kwenye hospitali ya Med Clinic
Middleburg ambako anaendelea na matibabu.
Kwa
mujibu wa Meneja wa Makhabane, Simphia Mathanjwa mwimbaji huyo hivi sasa ana
nafuu ingawa anaendelea na matibabu.
Mathanjwa
alisema Makhabane kwa kuwa mwaka 2013 alikuja Tanzania kwenye Tamasha la
Pasaka, ambako katika tamasha hilo
alionesha umahiri mkubwa kwa kuimba
nyimbo mbalimbali ambazo zilikonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo ambako
alitoa wito kwa Watanzania kumuombea dua kwa Mungu ili apate nafuu.
“Kwa
kuwa Watanzania wanatambua umahiri wa
Makhabane, tuunganishe nguvu pamoja kumuomba Mungu ampe nafuu ili arudi kwenye
njia ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu,” alisema Mathanjwa.
Aidha
Sipho ni mmoja wa waimbaji wanaotajwa na mashabiki wa muziki huo hapa nchini, ambaye atashiriki
kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.
Pamoja
na tukio hilo, Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka inaendelea kufuatilia taarifa za mwimbaji
huyo na inazidi kumuombea Makhabane
apone haraka.
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions , Alex Msama anampa pole
mgonjwa ambaye naye alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kuunganisha nguvu
ya pamoja kwenye maombi.
Katika
hatua nyingine, Msama Promotions, inajipanga kuwapeleka wawakilishi wawili kwenda Afrika Kusini kumjulia hali
Makhabane ambao ni Hudson Kamoga na
Jimmy Rwehumbiza.
No comments:
Post a Comment