HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 27, 2015

WANACHI WALALAMIKIA UGUMU WA MAISHA LICHA YA KUWA NA RASILIMALI ZA KUTOSHA

 William Mungai ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
 Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la Mufindi Kaskazini.

Na Mwandishi Wetu

Wananchi wa wilaya ya mufindi  mkoani Iringa wamelalamikia ugumu wa maisha wanaokumbana nao kila kukicha licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali ya misitu pamoja na mazao ya biashara

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wilayani mufind Williamu Mungai mmoja wa wananchi hao Clement Mwachanga alisema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya inayofanya vema kwa kuingiza pato kubwa la taifa lakini wananchi wake wako katika wimbi kubwa la umaskini

Mwachanga amesema anashangaa wilaya kama ya mufindi inayoongoza kwa utoaji wa mbao nyingi lakini cha kushangaza shule nyingi  za msingi hazina madawati jambo linalopelekea wanafunzi wengi kukaa chinii

‘’Hii ni aibu kubwa sana kwa wilaya yetu haiwezekani wilaya inarasilimali za kutosha lakini wananchi wake wengine wanashidwa hata kupata mlo mmoja kwa siku huku watoto wao wakishidwa kupelekwa shule kutokana na kushidwa kulipa ada ya kumuandikishia mtoto ”

Kwa upande wake Williamu Mungai ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kulichukua jimbo hilo la mufindi kaskazi ambalo kwa sasa linaongozwa na naibu waziri wa maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa amewataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shule za msinga hata kama hawana ada ya kuandikishiwa kwa kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania

Mungai  alisema ni kila mtoto ana haki ya kupata elimu ya msingi kwa kuwa ndivyo katiba inavyosema   na kuwataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarudisha majumba watoto kwa kisingizio cha kukosa hela ya kuwaandikishia
"Niwatake wenyeviti wangu wa mitaa muhakikishe watoto wote wanaandikiswa  na kama kuna mwalimu atagona kumuandikisha kwa kisingizio eti hana shilingi eflu hamsini jikusanyeni pamoja niiteni na mimi twende wote tuone kama hata muandikisha kwa maana walishasema elimu bure sasa bure waliyosema ikuwapi" alisema Mungai

Hata hivyo mungai alisema imefika wakati wakuikomboa mufindi iliyoko katika wimbi la umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuataka wanamufindi kuhakikisha  wanachagua viongozi wenye maono ya mbali katika kuwalete maendeleo na sio porojo za kila siku.

Mungai alisema kuwa  atahakikisha anazunguka vijiji vyote 72 vya wilaya ya mufindi katika harakati zake za kujenga chama na kuweza kutambua kero za wananchi na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua.

No comments:

Post a Comment

Pages