Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara atakuwa mgeni rasmi
kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Taifa Wanawake kati ya Pwani na Temeke
itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni itachezeshwa na mwamuzi wa FIFA, Jonesia
Rukyaa, na itaonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam. Waamuzi wasaidizi
ni Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamishna ni
Ingridy Kimario.
Timu za
Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia
saa 8.00 mchana. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin na
kufanyika kwa mara ya kwanza nchini atapata kombe na sh. milioni tatu.
Makamu
bingwa atapata sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu atapata sh. milioni
moja. Kiingilio kwenye mechi hizo ni bure.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment