BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki nchini, Dully Sykes,
Ebby Sykes amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto wake wa kike aitwaye Raya Sykes
amethibitisha taarifa hizo kwenye mtandao wa Instagram.
Raya katika ukurasa wake huo aliandika ‘Mungu akulaze
mahala pema peponi baba angu mimi nilikupenda lakini Mungu alikupenda
zaidi…nasikitika nipo mbali sitaweza kukuzika. Ulikuwa ni mtu mwenye upendo na
kila mtu alikupenda, nakupenda sana baba angu RIP dady nitakukumbuka milele
daima’.
Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa
kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae.
Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka
huu alikuwa anatimiza miaka 63.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe….
No comments:
Post a Comment