MGOGORO uliyokwamisha mradi mkubwa wa maji
katika vitongoji vya Liwale na Kwamsamati, vilivyoko mtaa wa Luguluni Kata ya
Kwembe wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam sasa umepatiwa suluhu.
Mradi huo, unagharimiwa na Kampuni ya Majitaka
na Majisafi, Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, huku wananchi wakichangia kidogo
kumalizia mita 200 hadi 450 zilizobaki kufika katika vitongoji hivyo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara
uliyofanyika juzi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Abdulhaman Said, alisema kuchelewa kukamilika kwa mradi huo
kulitokana na mradi huo kuwa na kamati tatu ambazo zimezua maswali kwa wanachi.
Suluhu ya mgogoro huo ilipatikana juzi baada ya
mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo kukubaliana na wananchi kuchagua wajumbe
wanane wa Kamati ya Maji ya vitongoji hivyo ambapo kila upande wa utatoka
wajumbe wanne.
Wajumbe hao ni Shamne Liperatusi Elizabeth
Isihaka, Vicent Makundo na Mogosi Shingilila hawa ni kutoka mtaa wa Liwale.
Wengine kutoka Kwamsamati ni Shomari Diwaga,
Hippy Kihiyo, Coletha Paul na Edgar Jave.
“Hatukuja hapa kuvunja kamati yenu iliyokuwepo
awali bali tumekuja hapa kuchagua kamati moja ambayo itakuwa na baraka
zote za wananchi,”alisema Said.
Said, alisema serikali ya mtaa huo iliamua
kufanya hivyo ili kuondoa aibu kwamba viongozi wa mtaa huo ndio wanaokwamisha
mradi huo huku wananchi wakiteseka.
Aidha, baada ya kumilika kazi ya kuchagua
Kamati hiyo, wanatarajia kuanzia jana wangekamilisha utiaji saini wa barua na
muktasari iliyokuwa ipelekwe Dawasco kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ili
wananchi waanze kupata maji.
Ofisa Mtendaji, Ramadhan Kanuwa, aliwataka
wajumbe wa Kamati hiyo kujipanga haraka ili waweze kwenda kufungua Akaunt Benki
jambo ambalo ni muhimu mno kwa jumuiya ya watumia maji.
No comments:
Post a Comment