HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 20, 2015

PINDA ASITISHA ZIARA KWA MAZISHI YA ASKOFU

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Peter Pinda, amelazimika kusitisha ziara yake kwa siku moja Mkoa wa Iringa kutokana na mazishi ya aliyekuwa Askofu Mstaafu Magnus Mwalunyungu.

Waziri Pinda ana ziara ya siku nne yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Iringa.

Akiwa katika mazishi ya Askofu huyo, Waziri Mkuu alisema angekosa amani kama asingehudhuria katika shughuli hiyo muhimu ambayo hata Rais wa nchi ametuma salama za rambirambi.

"Poleni wana Iringa na kanisa kwa ajumla kwa Kupoteza mzee huyu na tumuombee marehemu" alisema Waziri Mkuu.

Alitumia fursa hiyo pia kuwataka maaskofu na kanisa kutoa ushirikiano baina yao na Serikali kwa ajili ya kutoa kuwafanya Wananchi kuwa mfano bora, waadilifu wenye hofu ya Mungu na mambo yabadilike.

No comments:

Post a Comment

Pages