HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2015

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMA ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA ILIYOPOTEZA WATU SITA KATIKA AJALI YA MOTO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya (wa tatu kulia) wakiomboleza msiba wa familia ya watu sita waliofariki kwa ajali ya moto juzi. 
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), David Mpila aliyefariki pamoja na familia yake kwa ajali ya moto ulioteketeza nyumba yake usiku wa kuamkia Februari 7 eneo la Kipunguni ‘A’ jijini Dar es Salaam. Familia hiyo inazikwa Jumanne Februari 10 katika makaburi ya Airwing, Ukonga. 
Msemaji wa Familia, Godfrey Mwandosya

Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi  kwa Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiq kutokana na vifo hivyo vya watu sita wa familia moja waliopoteza maisha kwa moto usiku wa kuamkia jana, Jumamosi, Januari 7, 2015, katika eneo hilo  la Kipunguni ‘A’, Ukonga.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amevielezea vifo hivyo kuwa ni vya kusikitisha na kuhuzunisha sana.

“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya vifo vya watu sita wa familia moja kutokana na kuunguzwa na moto.

Ni vifo vya kusikitisha na kuhuzunisha sana. Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza pamoja nawe, ndugu na jamaa na Wanaukonga wote kwa msiba huu mkubwa na wa ghafla,”alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Naomba uniwakilishie salamu zangu na pole nyingi kwa Wanafamilia, wanandugu na jamaa wote ambao wamepoteza wapendwa wao katika tukio hili. Wajulishe kuwa niko nao na naungana nao katika kuomboleza vifo vya wapendwa wetu hawa kwa sababu msiba huu ni wetu sote. Aidha, waambie kuwa naungana nao katika kumwomba mwenyezi mungu, mwingi wa Rehema, aziweke pema roho za marehemu.”



Rais Kikwete pia aliongeza kuwa ni matarajio yake kuwa vyombo husika vya Serikali vitafanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo ili kubaini chanzo na mazingira ya moto huo.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi leo limekabidhi miili ya marehemu sita wa familia moja kwa ndugu zao kwa ajili mazishi, yanayotarajiwa kufanyika Februari 10 katika makaburi ya Air Wing Ukonga wilayani Ilala jijini Dar es Salaa.

Watu hao sita ni Kepten  mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), David Mpila na familia yake walifariki juzi kwa kutetekea kwa moto eneo la Kipunguni ‘A’ katika Wilaya hiyo jijini.

Mbali na Kepteni Mpila, wengine waliofariki dunia katika tukio hilo la moto ni mkewe, Celina Yegela na watoto wao; Lucas Mpila na Samwel Yegela  wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-30 pamoja na wajukuu Celina Emmanuel (9) na Paulina Emmanuel (5).
Familia hiyo ilitekelea kwa moto usiku wa kuamkia juzi, inadaiwa chanzo cha moto ilikuwa ni hitilafu ya umeme baada ya watu waliokuwa wakiangalia mpira sebuleni kushindwa kuzima vifaa vya umeme walipokwenda kulala.

Msemaji wa familia ya marehemu Mpira, Godfrey Mwandosya, alisema miili baada ya kukabidhiwa itaendelea kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi Jumanne asubuhi Februari 10 itakapotolewa kwa ajili ya mazishi katika makaburi hayo.

Alisema hatua hiyo inatokana na kuwa tangu familia hiyo ilipoteketea uangalizi wake ulikuwa chini ya jeshi hilo la polisi, ambalo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo.

Alisema miili ya marehemu itawasili nyumbani kuanzia saa 5  asubuhi na baadaye itafuata ibada ya kuaga miili hiyo na saa nane mchana wataelekea katika Kanisa Katoliki la Ukonga kwa ajili ya ibada ya kuwaombea marehemu na kisha kuelekea makaburini.

“Unajua kwa vile mzee alikuwa mwananajeshi, kwa utaratibu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania inapotokea tatizo kama hili linawajibika kusimamia mazishi kwa hiyo katika msiba huu litawajibika kwa watu watatu wengine ni juu ya familia,”alisema Mwandosya.

Aidha, alisema mtoto wa marehemu aliyenusurika na ajali hiyo ya moto, katika ajali hiyo, watoto wawili waliopoteza maisha ni wakwake, bado amehifadhiwa mbali na eneo la tukio, kwani ana matatizo ya kichwa pamoja na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).
“Tunaishukuru sana serikali kwani tangu juzi imekuwa mstari wa mbele katika kutoa vyakula,”alisema Mwandosya.

No comments:

Post a Comment

Pages