Timu ya Taifa ya Tanzania
ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na ushindi wa mabao
5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo uliofanyika
kwenye Uwanja wa fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini Mombasa.
Katika mchezo huo mabao
ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne na Mwalimu Akida bao moja .
Kipindi cha kwanza kilimazika
kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya
3 na kipindi cha tatu na cha mwishokwa mchezo kimalizika kwa Tanzania kupata
mabao 5 Kenya 3.
Mechi ya marudiano
inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam,
na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya, itacheza na timu
ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.
Mchezo wa kwanza
utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano
yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.
Timu inarejea leo jijini
Dar es salaam majira ya saa 11 jioni ikitokea jijini Mombasa nchini Kenya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment