Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko mbioni kupata mdhamini wa Ligi Daraja la
Kwanza (FDL). Tunatarajia mdhamini huyo atakuwa tayari kwa ajili ya msimu wa
2015/2016.
Ligi
Daraja la Kwanza inashirikisha timu 24 zinazocheza katika makundi mawili ya
timu 12 kila moja kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Timu
zinazocheza FDL msimu huu ni African Lyon (Dar es Salaam), African Sports
(Tanga), Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Faso (Morogoro), Friends
Rangers (Dar es Salaam), Geita Gold (Geita), Green Warriors (Dar es Salaam), JKT
Kanembwa (Kigoma), JKT Mlale (Ruvuma) na JKT Oljoro (Arusha).
Nyingine
ni Kimondo (Mbeya), Kinondoni Municipal Council (Dar es Salaam), Kurugenzi
(Iringa), Lipuli (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga), Panone FC
(Kilimanjaro), Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora,
Rhino Rangers (Tabora), Toto Africans (Mwanza), na Villa Squad (Dar es Salaam).
KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA
500,000/-
Kipa bora
wa michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake, Belina Julius wa Temeke amezawadiwa
sh. 500,000 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella
Mukangara.
Dk
Mukangara alitoa zawadi hiyo baada ya mechi ya fainali ya michuano
iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es
Salaam. Dk Mukangara alikuwa mgeni rasmi kwenye fainali hiyo.
Temeke
ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza
nchini baada ya kuilaza Pwani bao 1-0 katika fainali iliyoonyeshwa moja kwa
moja (live) na televisheni ya Azam.
Ilala
ilifanikiwa kutwaa baada ya kuichapa Kigoma mabao 3-0. Bingwa amepata sh.
milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu ameondoka
na sh. milioni moja katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Proin.
MECHI ZA MWISHO FDL SASA FEB 8 NA 10
Mechi za raundi mbili za mwisho za Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kwa makundi yote mawili zimerudishwa nyuma kutokana na
maombi ya klabu hizo kupungaza gharama za kuendelea kuziweka kambini timu zao.
Hivyo, Februari 8 mwaka huu kundi A litacheza
mechi zake za raundi ya 21 wakati zile za raundi 22 ambayo ndiyo ya mwisho
zitafanyika Februari 13 mwaka huu. Mechi za Februari 8 ni KMC vs African Lyon,
Kurugenzi vs African Sports, Majimaji vs JKT Mlale, Kimondo vs Friends Rangers,
Ashanti United vs Villa Squad, Polisi Dar vs Lipuli.
Februari 13 mwaka huu ni African Lyon vs
Polisi Dar, Kurugenzi vs Lipuli, Kimondo vs Majimaji, JKT Mlale vs Ashanti
United, Friends Rangers vs African Sports, na Villa Squad vs KMC.
Kwa upande wa kundi B wataanza mechi za
raundi 22 Februari 10 mwaka huu ili kupisha mechi za viporo za Polisi Mara
zinazomalizika Februari 5 mwaka huu. Hivyo, Februari 10 mwaka huu itakuwa ni
Burkina Faso vs JKT Kanembwa, Mwadui vs Polisi Tabora, Polisi Dodoma vs Green
Warriors, Rhino Rangers vs JKT Oljoro, Panone vs Polisi Mara, Geita Gold vs
Toto Africans.
Raundi ya 22 itachezwa Februari 15 mwaka
huu kwa mechi kati ya JKT Kanembwa vs Green Warriors, Mwadui vs Burkina Faso,
Polisi Tabora vs JKT Oljoro, Polisi Dodoma vs Panone, Toto Africans vs Rhino
Rangers, na Geita Gold vs Polisi Mara.
RAMBIRAMBI MSIBA WA KATIBU IRFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA), John Ambwene Mwakalobo uliotokea jana
(Februari 1 mwaka huu) mkoani Iringa baada ya kuanguka akiwa nyumbani kwake.
Msiba huo ni pigo kwa wadau wa mpira wa
mpira wa miguu kwani wakati wa uhai wake, Mwakalobo alitoa mchango mkubwa akiwa
kiongozi. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa IRFA, kabla ya 2012
kushinda nafasi ya Katibu Msaidizi.
Alizaliwa Februari 4, 1954 na kupata
elimu ya sekondari katika shule ya Azania, Dar es Salaam na baadaye mafunzo ya
ualimu kwenye Chuo cha Ualimu Mpwapwa mkoani Dodoma. Alianzia kazi ya ualimu
Newala mkoani Mtwara kabla ya kuhamia mkoani Iringa mwaka 1981. Alistaafu mwaka
2013.
TFF inatoa salamu za rambirambi kwa
familia ya marehemu, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa msiba huo.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho (Februari
3 mwaka huu) kwao Kyela mkoani Mbeya. Ameacha mke, watoto wanne na mjukuu mmoja.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment