Rais wa Shrikisho
la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na ushindi wa mabao
4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).
Katika salam zake
Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo huo wa awali,
umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian
Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.
Aidha Rais
amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata, bali
wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili waweze
kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Mchezo wa marduiano
unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam
na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la
Wanawake (All Africa Games Women) zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18
mwaka huu.
Twiga Stars
inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam kwa
usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia
ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa
pongezi Twiga Stars kwa ushindi
walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.
Mabao ya Twiga
Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo) yalifungwa na
Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
BEACH SOCCER YAREJEA LEO Wakati huo timu ya
Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) inarejea leo mchana saa 8:45,
kwa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Misri ambapo jana ilipoteza
mchezo wake wa marudiano kwa kufungwa 9-4 na wenyeji.
Rais Malinzi
amesema timu ya Soka la Ufukweni haikupata matokeo mazuri katika mchezo wake
kutokana na ugeni wa michuano hiyo, uzoefu ndio ulikuwa kikwazo kwa timu ya
Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ikiwa ni miezi sita
tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini Tanzania.
Ili kuwa na timu
bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF limepanga kuutangaza na kuufundisha mpira wa ufukweni katika mikoa
mbali mbali nchini Tanzania, tofauti na sasa ambapo mchezo huo unachezwa Dar es salaam na Zanzibar.
Katika mchezo wa
jana mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi (3) Kashiru Salum (1), Tanzania
imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za Soka la Ufukweni barani Afrika na Misri
kwa jumla ya mabao 15-6.
Misri imefanikiwa
kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la Ufukweni Visiwa vya Shelisheli,
zitakazofanyika mwezi April mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa
kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment