Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (kulia) akitoka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo huku akiambatana na wanasheria wake, John Mallya (kushoto) na Nyaronyo Kicheere ambapo aliandika maelezo na kuhojiwa na Polisi kwa saa sita kuhusiana na tuhuma za kutaka kuuwawa na mlinzi wake, Khalid Kagenzi. (Picha na Francis Dande)
Dk. Willibroad Slaa akiizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maeleza na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kituo Kikuu cha Kati.
Dk. Willibroad Slaa akiizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maeleza na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kituo Kikuu cha Kati.
Mlinzi mpya wa Dk. Willibrod Slaa akimfungulia mlango.
Na Mwandishi Wetu
Dk. Willibroad Slaa akiizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maeleza na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kituo Kikuu cha Kati.
Mlinzi mpya wa Dk. Willibrod Slaa akimfungulia mlango.
Na Mwandishi Wetu
SIKU mbili baada ya kuwachiwa mtuhumiwa Khalid Kagenzi anayedaiwa
kutaka kumuuwa kwa sumu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), hatimaye Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa, naye
amehojiwa leo.
Dk. Slaa alifika Kituo Kikuu cha Kati majira ya saa nne asubuhi kwa
ajili yakuhojiwa na kuandika maelezo kuhusu tukio lakutaka kuuawa kwa kulishwa
sumu.
Katika mahojiano hayo, Dk. Slaa aliongozana na wanasheria wake
Nyoronyo Kicheere na John Malya, yalichukuwa muda wa saa sita huku baadhi ya
wananchama waliombatana naye wakimsubiri mnje.
Baadhi ya viongozi aliyoongozana nao walikuwa ni Profesa Abdallah
Safari ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara, Godbles Lema na John
Heche.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza mahojiano
hayo, Dk Slaa, alisema kuwa maelezo hayo yatumika katika ushahidi kuhusu tukio
hilo.
Aidha Diwani Ubungo (Chadema), Jocob Boniface, alikuwa akihojiwa hata
hivyo hadi waandishi wanaondoka katika eneo hilo alikuwa hajotoka kituoni hapo.
Kufikishwa katika kituo hicho kumetokana na sakata Chadema kutoa
tarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kulikuwa na mpango wa mlinzi wake
Kagenzi kutaka kumuua kwa sumu.
No comments:
Post a Comment