Meneja
wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula kwa
wahanga wa mafuriko Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (Kushoto) akipokea msaada
kutoka kwa Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru (Kulia)
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) yakabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama. Msaada uliotolewa ni pamoja na mchele kilo 740, unga kilo 600, maharage kilo 300 na mafuta ya kupikia lita 260.
Msaada huo umekabidhiwa na
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt. Kamugisha Kazaura.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL
Bw. Peter Kuguru alisema TTCL inawapa pole sana wahanga wa tukio hilo na kwamba
TTCL imepokea kwa huzuni kubwa tukio hilo na kuwataka Watanzania kuwaombea
waliopatwa na janga hilo wapate faraja na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu
waliopoteza maisha awapumzishe mahali pema peponi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.Benson Mpesya akizungumza
baada ya kupokea msaada huo, aliishukuru TTCL
kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa mvua hiyo na kuongeza kuwa
TTCL wamekuwa na moyo wa huruma kwa wahanga hao huku akiahidi kuwa misaada
inayotolewa na watu wenye mapenzi mema itatumika kwa wahanga wa tukio hilo na
si vinginevyo na atakuwa mkali kwa hilo.
No comments:
Post a Comment