HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2015

TWIGA YAWAPA WATANZANIA MATUMAINI

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Selestine Mwesigwa (kulia) akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili (kushoto) kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume, Ilala anayeshuhudia katikati ni  kocha wa Twiga Stars Rogasian Kaijage. 
Kikosi cha timua ya Taifa ya wanawake, ‘Twiga Stars’ wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Soka la wanawake Tanzania, (TWFA) na uongozi wa  TFF pamoja na benchi la ufundi baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa tayari kwa safari ya Zambia kucheza mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za wanawake barani Afrika
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
KOCHA wa timu ya Taifa ya wanawake, ‘Twiga Stars’ Rogasian Kaijage na nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili wameahidi ushindi kwenye mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za wanawake barani Afrika utakaochezwa jumapili nchini Zambia.

Twiga ambao wameingia hatua ya pili kutokana na kuwa kwenye nafasi za juu kwenye viwango vya ubora barani Afrika itakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Zambia ambao ndio waliowaondoa kwenye mashindano hayo mwaka jana.

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wakiagwa na Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Selestine Mwesigwa, Kaijage alisema ana kikosi kizuri na chenye hari ukilinganisha na mwaka jana kwani wamepata muda wa mafunzo wa kutosha.

“Mwaka huu nina kikosi kizuri na chenye ari tofauti na mwaka jana na nimepata muda wa kutosha wa kuwafundisha japo sikupata mechi za kimataifa za kirafiki lakini nimetumia njia mbadala kuhakikisha nafanikisha lengo langu”, alisema Kaijage.

Naye nahodha wa timu hiyo, mkongwe Sophia Mwasikili alisihi watanzania wakuwaombea dua ili wapate ushindi na wao watafanya kila wawezalo na kutumia ujuzi ambao kocha amewapa kuhakikisha wanapata ushindi.

Twiga Stars itaondoka kesho alfajiri na ndege ya Shirika la Ethiopia ‘Ethiopia Airways’ na itapitia Ethiopia  ikiwa na msafara wa watu 25 ambao ni na Blassy Kiondo (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji), Beatrice Mgaya (kiongozi msaidizi), Rogasin Kaijage (kocha mkuu), Nasra Juma (kocha msaidizi), Furaha Francis (Meneja), Christine Luambano (Daktari) na Mwanahamis Abdallah (Mtunza vifaa).

Wachezaji ni Asha Rashid, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Donisi Minja, Amina Bilal, Fatuma Bashiri, Esther Chabruma, Shelda Mafuru, Maimuna Kaimu, Najiat Abbas, Stumai Abdalla, Fauma Issa, Thereza Yona, Fatuma Hassan, Fatuma Omary, Sophia Mwasikili, Fatuma Khatibu na Etoe Mlenzi.

No comments:

Post a Comment

Pages