March 31, 2015

Ukatili wa Mwekezaji Mtibwa wawapeleka, Wafanyakazi kwa Waziri Mkuu

Na Bryceson Mathias

UNAODAIWA ni Ukatili wa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa Morogoro, umewakasirisha Wafanyakazi wa Kiwanda hicho na kuwasababishia leo watinge bungeni Dodoma kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kumshitaki wakilalamikia Unyama wanaofanyiwa.

Wakionesha Sekula Na.C.1/18//2015 ya 22/3/2015 iliyonakiliwa kwa Wakuu wa Idara wa Kapumpuni hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU) na Mbao za Matangazo kwa wafanyakazi wote, wamedai ukatli huo hautekelezeki.

“Kutokana na Ukatili na Unyama aliotufanyia mwekezaji kututaka tujaze fomu ya kufanya kazi kwa malipo ya kuchelewa kuanzia Mei hadi Juni mwaka huu, na wasiotaka kujaza fomu hizo wajaze likizo bila malipo ili wafanye shughuli zingine, ni kutufukuza kazi kienyeji".

“Hatua za kututaka tujaze fomu hizo kuanzia 26/03/2015 na kurudisha ofisini kabla ya 1/4/2015 saa mbili, na kwamba mfanyakazi ambaye hatajaza kati ya fomu hizo kufanya kazi kwa malipo ya kuchelewa au likizo bila malipo ndani ya siku tano atakuwa amejifukuzisha ni ukatili” walisema wafanyakazi.

Kufuatia Tangazo hilo Maalum ambalo limesainiwa na Kaimu Meneja Rasilimali, VT Mazengo na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Mtibwa, Hamad Yahaya, wafanyakazi hao wamekasirishwa na hawakuridhishwa nalo, na hivyo baada ya Kikao wameamua Kutinga kwa Pinda bungeni.

Katika Msafara huo wa Watu Watano, wamo viongozi wa Chama cha Wafanyakazi (TPAWU), Uongozi wa Wakulima Wadogo wa Miwa, Diwani wa Kata ya Mtibwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Luka Mwakambaya.

Aidha mapema kabla ya hatua ya Wafanyakazi hao, walipiga Kambi kwenye lango la mwekezaji kudai malipo  na Mishahara ya mwezi wa 12. 2014 na Februai 2015, ambapo pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero kumtaka Mwekezaji awalipe, hakutekeleza, hatua ambayo wafanyakazi na Wakulima wanaona amefirisika, Serikali ipeleke mwekezaji Mpya.

No comments:

Post a Comment

Pages