March 31, 2015

WAENDESHA BODABODA NA BAJAJ MBEYA KUNUFAIKA NA MIKOPO YA PIKIPIKI NA BAJAJ INAYOTOLEWA NA BENKI YA CRDB

Waendesha bodaboda na Bajaj mkoani Mbeya wakiwa katika mkutano wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo ya Pikipiki na Bajaji inayotolewa na Kampuniya CRDB Microfinance Services. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB. Dk.Charles Kimei akimkabidhi mwendesha bodaboda koti maalum kwa ajili ya usalama, Matokeo Swalo, mkazi wa mjini Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo ya Pikipiki na Bajaji inayotolewa na Kampuniya CRDB Microfinance Services. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Nyerembe Munasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB. Dk.Charles (kushoto akimkabidhi kofia ngumu mwendesha bodaboda, Ponzi Manga mkazi wa mjini Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo ya Pikipiki na Bajaji inayotolewa na Kampuni ya CRDB Microfinance Services. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Nyerembe Munasa.

Na Esther Macha, Mbeya

MKURUGENZI wa benki ya (CRDB) Dk. Charles Kimei amesema kuwa ili waendesha bodaboda waweze kuwa na maisha mazuri hawana budi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ambazo wanapata katika shughuli zao.

Amesema kuwa ili kila mtu aweze kufanikiwa katika maisha ni vema kuweka akiba ambayo nayo bila nidhamu ya matumizi huwezi kufika popote.

Dk. Kimei amesema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma ya  mikopo ya bodaboda ambayo inaendeshwa na benki ya CRDB maarufu kwa jina la (Jiendeshe) iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa uliopo jijini hapa.

Mkurugenzi huyo aliwataka waendesha bodaboda kuweka akiba hata kama wanapata kidogo ikiwa ni pamoja na kujiwekea malengo ya baadaye ili waweze kuwezesha shughuli zingine ambazo zitawawezesha kufanya miradi mingine.

“Ndugu zangu waendesha bodaboda mnapotumia fedha  lazima mkumbuke  kesho ,siyo unapata fedha unakimbilia kutumia katika masuala ya ulevi,mtu anayefanya hivyo ujue hawezi kuwa tajiri kutokana na kuwa na matumizi mabaya ya fedha na pamoja na kutojiwekea malengo”alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha Dk. Kimei aliwataka waendesha bodaboda hao kama wanaona kuwa biashara hiyo inakuwa na ushindani mkubwa ni vema wakabuni biashara nyingine ambayo inaweza kuwa mbadala kwao.

“Najua hivi sasa  kwa uzinduzi huu wa huduma za mikopo ya boaboda biashara hii itakuwa na ushindani mkubwa sana hivyo kama mkiona ushindani umekuwa mkubwa jipangeni na kuanzisha miradi mingine ambayo itawawezesha  kuendesha maisha yenu”alisema.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa CRDB Microfinance  benki,Sebastian Masaki alisema kufunguliwa kwa wodi maalum kwa ajili  waendesha bodaboda si jambo zuri  na kwamba asilimia 66 ya bajeti ya hospitali ya Mbeya huwa inatengwa kwa ajili ya ajali za bodaboda.

Alisema masuala ya ajali yasiwepo tena kwa waendesha bodaboda hivyo kikubwa waelimishwe kuhusu ujasiriamali.

Naye Katibu wa waendesha bodaboda Mkoani Mbeya Msumba Mbesa alisema kutokana na kuwa na mazingira magumu ya biashara imewapelekea kufanya kazi mpaka usiku wa manane ili waweze kufanikisha malengo ya fedha za matajiri wao.

Alisema kwa hii mikopo ambayo Benki ya CRDB watakabidhi kwa waendesha bodaboda ambazo watakuwa wanamiliki wenyewe zitaweza kusaidia waendesha bodaboda hao kumiliki za kwao.

No comments:

Post a Comment

Pages