April 03, 2015

Waimbaji kutoka Uingereza watua kunogesha Tamasha la Pasaka

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza leo. (Picha na Loveness Bernard)
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza leo. 
 Kutoka kushoto, Angela Kaonja, Nyakwesy Mujaya na Grace Khuni
 Angela Kaonja akimvisha skafu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
 Nyakwesy Mujaya akimpa au mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi, akipokea ua kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Msama Promotions, Nyakwesy Mujaya, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka. Kulia ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.

 Msama akipeana mkono na Ifeanyi Kelechi,
 Msama akiteta jambo na Ifeanyi Kelechi,
 Ifeanyi Kelechi akiimba moja ya nyimbo zake.
 Ifeanyi Kelechi akiimba.
 Miller Luwoye.
 Anthonia Nwafor.
 Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama (wa pili kulia) akiwa na waimbaji kutoka Uingereza.

NA LOVENESS BERNARD

MWIMBAJI wa kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Uingereza, Ifeanyi Kelechi, ametua nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili.
Kelechi, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jana saa mbili asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar, akiongozana na wenzake wanne.


Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Kelechi alisema lengo la ujio wake ni kuhakikisha tamasha hilo linanoga kuliko yaliyowahi kufanyika, ndio maana amekuja na jopo la waimbaji watano.


"Namshukuru Mungu kutufikisha salama, nimefurahi sana kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, hasa kuja kuimba kwenye tamasha kubwa kama hili, ambalo naamini litakuwa chachu ya kumfanya kila mtu kuvutiwa nalo," alisema.


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuzidi kumiminika kwa waimbaji, kunaashiria tamasha hilo litanoga zaidi.

"Waimbaji wetu wameshaanza kuwasili nchini na kesho waliobakia watawasili...Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa, tunaisubiria siku hiyo tu,” alisema Msama.
 
Tayari muimbaji Faustine Munishi ‘Malebo’ mtanzania anayeishi nchini Kenya tayari kawasili tangu juzi huku Ephraim Sekeleti wa Zambia, Rebecca Malope na Solly Mahlangu ‘Obrigado’ kutoka Afrika Kusini watafuata.

Mbali na waimbaji hao kutoka nje, watakuwepo pia wakali wa hapa nchini wakiwamo Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro na wengineo.

No comments:

Post a Comment

Pages