April 02, 2015

WACHUNGAJI WATAKIWA KUWARUHUSU WAUMINI KUHUDHURIA TAMASHA LA PASAKA

Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel  ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama. (Picha na Francis Dande)

Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas hilo.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas la Pasaka. Kulia ni Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel  ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota.

NA LOVENESS BERNARD

Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly,  David Mwasota amewataka wachungaji wote nchini  kuwaruhusu waumini wao kuhudhuria katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika April 5 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Askofu huyo amewataka wachungaji wawaruhusu waumini waweze kusherehekea kufufuka kwake Yesu kristo kwa kusifu  na kuabudu pamoja na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
 
Nawaomba wachungaji wawaruhusu waumini baada ya ibada waje uwanja wa taifa tumsifu muumba wa vyote kwa nyimbo na sala pamoja na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama alisema waimbaji wameshaanza kuwasili nchini wakiongozwa na Faustine Munishi (Malebo) ambaye aliwasili jana huku Kerechi muimbaji kutoka Uingereza  akitarajiwa kuwasili Jumamosi.

Maandalizi tumekamilisha kwa asilimia 99 na waimbaji wameanza kuwasili nchini ambapo Faustine Munishi mtanzania aishie nchini Kenya na kesho tunatarajia kumpokea Ifeanyi Kerechi na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia huku Rebecca Malope na Solly Mahlangu tukuwatarajia kuwasili Aprili 3 alisema Msama.

No comments:

Post a Comment

Pages