HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2015

Akamatwa na Risasi 10 Kibindu, wanne watoroka

Na Bryceson Mathias, Kibindu

MTU mmoja amekamatwa ndani ya msitu wa Kata ya Kibindu aliyefahamika kwa jina la Ally Ayubu ambaye licha ya kukutwa na kisu pia alipopekuliwa alikutwa na risasi 10.


Katibu Mtendaji wa Kijiji cha Kibindu, Juma Mgaza, amesema kuwa kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na taarifa zilizotolewa na mkulima mmoja baada ya kukutana na watu wasiofahamika katika kijiji hicho. 

Kutokana na Elimu waliyopewa Wananchi na Viongozi na Polisi, Mkulima huyo aliwaomba akatafuta Vocha ili apige simu kwa wenye Bodaboda waje wawasaidie, na walipobaini anawasiliana na Uongozi, walimwambia wao wanatangulia kwa Mguu asaidiwe Mgonjwa, wakatokomea porini.

Uongozi wa Kijiji ulipofika na kumhoji, alisema yeye anaitwa, Ally Ayubu, Mwenyeji wa Mkoa wa Singida, ambapo alipopekuliwa alikutwa na Risasi 10 ambazo hakutaja ni za bunduki aina gani, na Mahindi Mabichi yaliyovunjwa mashambani, na kuropoka kwamba kuna wenzake wenzao wawili wako porini wakiwa na bunduki moja.


Mgaza alisema, baada ya Polisi wa Kituo cha Pera kumchukua mtuhumiwa huyo na kuondoka naye hakukuwa na tukio lolote, na hakuna Mwananchi yeyote aliyetoa taarifa ya kuibiwa chochote, isipokuwa Mahindi wanavunja na Kula sababu ya Njaa.


“Sina Mwananchi yeyote katika Serikali yangu ya Mji Mdogo wa Madizi, ambaye amekamatwa na Polisi, kwa sababu mara baada ya kupata taarifa hizo, uongozi uliamua kupita kwa kila Mjumbe wa Mtaa kujua jambo hilo, lakini mtu yeyote ambaye alionekana kupotelewa na ndugu, isipokuwa Wakulima waliorudi toka mashambani Njeura”.alisema Ahmad.

No comments:

Post a Comment

Pages