Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema dhumuni la
huduma hiyo ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua
jezi popote walipo nchini.
Aveva alisema
klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake vya michezo nchi
nzima, hivyo mkataba huo abu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa
vyake vya michezo nchi nzima, hivyo mkataba huo utaongeza usaambazaji wa vifaa
vya michezo vya klabu hiyo.
“Klabu ya Simba
inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana
kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii kwa ajili
ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza
kununua mavazi na bidhaa za Simba kiurahisi na kwa bei nafuu” alisema Aveva.
Meneja wa Jumia
nchini Tanzania Jean –Philippe Boul alisema uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu
siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama
Simba.
Alisema katika
msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa
wapenzi wake kununua jezi za msimu huo, kupitia njia ya mtandao hivyo
wanajivunia kwa Aveva kuwachagua wao kwa kazi hiyo.
“Kupitia huu
umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa
Simba kuagiza jezi kuanzia leo(jana) mpaka Alhamisi Julai 31 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa
mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa rasmi kwa rejareja”.
“Tunawahamasisha
wapenzi wa Simba popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitia mtandao huu, kuona
urahisi katika kufanya manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaweza
kuagiza jezi kupitia tovuti ya jumia na kuletewa mzigo wako mpaka mlangoni.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited, Imani Kajula ambao ni
washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema
“kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongeza mapato yake
pia kudhibiti bidhaa feki,”.
No comments:
Post a Comment